Mar 02, 2024 07:31 UTC
  • Amnesty International yataka uchunguzi wa mauaji ya waliokuwa wakisubiria misaada Gaza

Shirika la Msamaha Duniani la Amnesty International limetoa wito wa kufanyika uchunguzi wa haraka kuhusu mauaji makubwa ya Wapalestina yaliyofanywa na utawala wa Kizayuni dhidi ya raia wa Gaza waliokuwa wakisubiria kupokea misaada ya kibinadamu katika Ukanda wa Gaza.

Shirika hilo la kimataifa la kutetea haki za binadamu limesema katika taarifa yake kwamba, kunapaswa kuweko uchunguzi wa haraka kuhusu habari za kutisha kwamba, makumi ya Wapalestina waliuawa na kujeruhiwa walipokuwa wakisubiri kupata msaada wa chakula kaskazini mwa Gaza.

Sehemu nyingine ya taarifa ya Amnesty International inasema: Watu wa Gaza wanakabiliwa na njaa, na Umoja wa Mataifa umetahadharisha mara nyingi kuhusu kutokea baa la njaa katika ukanda huo, na sababu kuu ya hali mbaya ya sasa ni mashambulizi ya kinyama ya Israel dhidi ya eneo hilo.

Wizara ya Afya ya Palestina jana ilitangaza kuwa wanajeshi wa Israel wamewauwa shahidi watu wasiopungua 104 waliokuwa katika umati uliokuwa ukisubiri kupatiwa misaada ya kibinadamu huko kusini mwa Gaza.

Wakazi wa Gaza wakipatiwa chakula cha msaada

 

Wakati walimwengu wakilaani jinai hiyo ya kinyama, Waziri wa utawala haramu wa Kizayuni wa Israel mwenye misimamo mikali ya chuki amewapongeza wanajeshi wa utawala huo walioua zaidi ya Wapalestina 100 waliokuwa wakisubiri misaada ya kibinadamu katika Ukanda wa Gaza uliowekewa mzingiro.

Itamar Ben-Gvir, anayeongoza wizara eti ya usalama wa taifa ya Israel amesema: "lazima tuwaunge mkono kikamilifu wapiganaji wetu mashujaa wanaoendesha oparesheni huko Gaza, ambao walichukua hatua barabara dhidi ya genge la watu wa Gaza ambao walijaribu kuwadhuru".

Tags