Mar 16, 2024 02:23 UTC
  • Borrell: Israel inafanya mauaji ya halaiki dhidi ya watu wa Gaza

Mkuu wa Sera za Kigeni wa Umoja wa Ulaya ambaye katika siku za hivi karibuni ameutuhumu utawala wa Kizayuni wa Israel kuwa unatumia "njaa kama silaha" katika vita vya Gaza, ameonya kuwa utawala huo unawaua watu wa Gaza kwa umati.

Katika mahojiano na kanali ya PBS ya Marekani, Josep Borrell amezungumzia mabadiliko ya maoni ya umma kuhusu vita vya Gaza na kupungua uungaji mkono wa kimataifa kwa utawala wa Kizayuni wa Israel na kuongeza kuwa: "Watu wana wasiwasi zaidi kuhusu kile ambacho kwa hakika naweza kukiita "mauaji ya halaiki. Takriban raia elfu 30 wameuawa na idadi hii ni kubwa sana."

Mkuu wa Sera za Kigeni wa Umoja wa Ulaya amesema: "Sisi katika Umoja wa Ulaya tumeainisha vipaumbele kuhusu suala la Palestina. Moja ya vipaumbele hivyo ni kutafuta suluhisho la nchi mbili na kuwapa Wapalestina haki ya kuwa na nchi na serikali yao.

Katika mahojiano hayo, Borrell amezungumzia pia mgogoro wa binadamu huko Gaza na kusisitiza kuwa, utawala wa Kizayuni wa Israel unatumia njaa kama silaha katika vita.

Gaza

Ameendelea kusema: "Mamia ya watu wanakufa kwa njaa, ikiwa ni pamoja na watoto wengi waliokufa kutokana na utapiamlo."

Amesema Wapalestina wa Gaza wanaaga dunia kutokana na hatua ya Israel ya kuzuia misaada ya kibinadamu kuingine eneo hilo.

Nchi za Ulaya na Magharibi kwa ujumla ambazo zimekuwa zikiuunga mkono na kuusaidia utawala katili wa Israel katika mauaji yake ya kimbari dhidi ya Wapalestina, zimeanza kujitoa kimasomaso na kukosoa uhalifu wa utawala huo katili kutokana na kushadidi mashinikizo ya umma ya kimataifa dhidi ya sera na siasa zao za kinafiki na kindumakuwili.  

Tags