Mar 22, 2024 11:46 UTC

Afisa usalama wa Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina HAMAS amepuuzilia mbali madai ya utawala haramu wa Israel kwamba makumi ya wanachama wa kundi hilo la mapambano ya Kiislamu wamekatwa na askari wa Kizayuni katika Hospitali ya al-Shifa katika Ukanda wa Gaza.

Kwa siku kadhaa mfululizo tangu Jumatatu, vikosi vya jeshi la utawala wa Israel vilivyojizatiti kwa silaha nzito vimeizingira Hospitali ya al-Shifa katika mji wa Gaza.

Afisa mmoja wa usalama wa HAMAS ambaye hakutaka kutaja jina lake ameiambia kanali ya televisheni ya al-Jazeera ya Qatar leo Ijumaa kuwa, kanda ya video iliyotolewa na Israel ikionyesha eti operesheni ya kukamatwa kwa wanachama wa HAMAS katika hospitali hiyo ni bandia na haikisi ukweli wowote.

Afisa huyo wa HAMAS amesema utawala wa Kizayuni umetoa na kusambaza mkanda huo wa video kama sehemu ya vita vyake vya kisaikolojia dhidi ya makundi ya muqawama katika Ukanda wa Gaza baada ya kushindwa katika medani ya vita.

Wakati huo huo, Harakati ya HAMAS leo Ijumaa imelaani kitendo hicho cha ukatili na kinyama cha utawala wa Kizayuni cha kuishambulia na kuizingira Hospitali ya al-Shifa huko Ukanda wa Gaza.

Askari hao makatili wa Kizayuni mbali na kuwauwa shahidi makumi ya raia wa Kipalestina katika Hospitali ya al-Shifa, lakini wamepelekea mamia ya wengine kuwa wakimbizi, huku wakiwazingira wagonjwa, waandishi wa habari, madaktari na wahudumu wa afya ndani ya hospitali hiyo. 

 Tokea Oktoba 7, 2023 hadi sasa, jeshi la Kizayuni limeshaua shahidi zaidi ya Wapalestina 32,000 wa Ukanda wa Gaza, wengi wao wakiwa wanawake, watoto na vijana wadogo.

Tags