Apr 26, 2024 03:09 UTC
  • Amir-Abdollahian: White House inapasa kusitisha haraka uungaji mkono wake kwa jinai za kivita za Israel

Akikosoa ukandamizaji na unyanyasaji wa askari usalama vya Marekani dhidi ya wahadhiri na wanafunzi wanaopinga jinai za kivita za utawala ghasibu wa Israel, Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesema: Ikulu ya Marekani inapasa kusitisha haraka iwezekanavyo uungaji mkono wake kwa jinai za kivita za utawala ghasibu wa Israel.

Fikra za waliowengi nchini Marekani zimekosoa pakubwa jitihada za Marekani za kuinasua Israel  katika kinamasi cha vita vya Gaza vilivyodumu kwa miezi saba sasa ambapo  Tel Aviv imegonga mwamba na kushindwa kutimiza malengo yake haramu. Katika siku za hivi karibuni wanafunzi wa vyuo vikuu nchini Marekani wamekuwa wakifanya maandamano kuwaunga mkono wananchi madhulumu wa Palestina na kupinga mauaji ya kimbari ya Israel dhidi ya Gaza. 

Maandamano na wanafunzi wa vyuo vikuu nchini Marekani katika kuonyesha mshikamano na kuwaunga mkono wakazi wa Ukanda wa Gaza na kutaka kusitishwa vita na mauaji ya kimbari ya Israe dhidi ya eneo hilo sasa yamefika hadi katika katika Vyuo Vikuu vya Havard, Texas, Brown na California Kusini; ambapo mapigano yameshuhudiwa kati ya polisi na wanafunzi katika Vyuo Vikuu vya Texas na California.   

Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Texas wakipambana na polisi 

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Hossein Amir -Abdollahian ameandika katika mtandao wa kijamii wa "X" katika radimali yake kwa vitendo vya ukandamizaji na mabavu vya polisi wa Marekani dhidi ya  wanafunzi wa  vyuo vikuu mbalimbali vya  nchi hiyo wanaoandamana  kuiunga mkono mkono Palestina kwamba: Walimwengu wamechukukizwa na kutiwa wasiwasi na ukandamizaji na ukatili unaofanywa na polisi na vikosi vya usalama vya Marekani dhidi ya wahadhiri na wanafunzi wanaoandamana kupinga mauaji ya kimbari na jinai za kivita za  utawala wa Israel dhidi ya Gaza.

Tags