Uungaji mkono mkubwa kwa mashambulio ya Hamas dhidi ya Israel
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i103214-uungaji_mkono_mkubwa_kwa_mashambulio_ya_hamas_dhidi_ya_israel
Mashambulio makubwa na ya kushtukiza ya nchi kavu, anga na baharini ya wanamapambano wa Kipalestina dhidi ya walowezi wa Kizayuni wanaokaliwa kwa mabavu ardhi za Palestina, yaliyopewa jina la Kimbunga cha Al-Aqsa yamepata uungaji mkono mkubwa wa kieneo na kimataifa.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Oct 08, 2023 08:05 UTC
  • Uungaji mkono mkubwa kwa mashambulio ya Hamas dhidi ya Israel

Mashambulio makubwa na ya kushtukiza ya nchi kavu, anga na baharini ya wanamapambano wa Kipalestina dhidi ya walowezi wa Kizayuni wanaokaliwa kwa mabavu ardhi za Palestina, yaliyopewa jina la Kimbunga cha Al-Aqsa yamepata uungaji mkono mkubwa wa kieneo na kimataifa.

Nchi zote za Kiislamu za eneo hili zikiwemo Afghanistan, Pakistani, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na hata nchi za Kiarabu za eneo kama vile Saudi Arabia zimeunga mkono mashambulizi hayo na kusema ni haki ya kisheria ya Wapalestina kujilinda dhidi ya jinai za utawala ghasibu wa Israel. Wakati ambapo Wazayuni walidhani kwamba wako salama katika jumba la kioo, wakitegemea msaada wa kijeshi wa Marekani, na wakati huo huo, kutarajia kwamba mchakato wa kuanzisha uhusiano wa kawaida na baadhi ya nchi za Kiarabu utabadilisha mlingano wa nguvu wa eneo kwa maslahi yao, mashambulio ya kasi ya umeme ya wanamapambano wa Palestina ambayo yamepelekea kuchukuliwa mateka maafisa wa ngazi za juu wa jeshi la utawala wa Kizayuni, yamethibitisha kwamba mahesabu yote ya Wazayuni yamekuwa ya makosa na kwamba kamwe hawatakuwa na amani wala usalama katika nyumba zao zilizojengwa katika ardhi zilizoporwa na kukaliwa kwa mabavu.

Ali Khazaei, mtaalamu wa masuala ya eneo anasema:

Maafa na idadi kubwa ya mateka wa Kizayuni waliochukuliwa na wapiganaji wa Palestina inaonyesha kuwa licha ya utawala huo unaokalia kwa mabavu Quds Tukufu kupewa zana za kisasa za usalama na kijeshi na nchi za Magharibi, hasa Marekani, lakini bado unaishi katika nyumba ya buibui, ambapo sasa wapiganaji wa Palestina kupitia mashambulizi yao makubwa ya kushtukiza, wamethibitisha kivitendo kwamba hata mifumo ya kiusalama na kijasusi ya utawala huo na ya waungaji mkono wake, haina nguvu wala uwezo wa kukabiliana na irada ya chuma ya Wapalestina.

Sehemu ya matokea ya Kimbunga cha al-Aqsa huko Israel

Uungaji mkono mkubwa wa kieneo na kimataifa, ukiwemo wa nchi za Jordan na Iraq, kwa mashambulizi ya wapiganaji wa Palestina dhidi ya maghasibu wa Israel unaonyesha wazi kwamba suala linaloainisha mustakbali wa kadhia ya Palestina na kubadilisha milingano ya nguvu, ni mtazamo wa fikra za waliowengi hususan katika nchi za Kiislamu, kuhusu utawala wa Kizayuni. Uungaji mkono mkubwa wa umma kwa mashambulizi ya wapiganaji wa Palestina unaonyesha kushindwa juhudi za utawala wa Kizayuni unaoungwa mkono kwa hali na mali na Marekani, na kwamba njama za kuanzisha uhusiano wa kawaida na baadhi ya watawala wa eneo, si tu si tiba kwa machungu ya Wazayuni, bali pia kunawasukuma kwenye mchakato wa upotoshaji ambao unawafanya wadhani kimakosa kwamba wameweza kuimarisha nafasi yao katika ardhi za Wapalestina wanazozikalia kwa mabavu kwa kujihusisha na mazungumzo ya kuanzisha uhusiano wa kawaida na baadhi ya nchi vibaraka za Kiarabu. Hii ni katika hali ambayo, mashambulizi ya karibuni ya pande zote ya wapiganaji wa Kipalestina yamevuruga kabisa dhana hiyo potofu na isiyo na msingi wowote wa kimantiki.

Khalid al-Qadoumi, Mwakilishi wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina Hamas nchini Iran anasema kuhusu suala hilo:

"Hatutaruhusu mtu yeyote kukanyaga wala kuchezea haki za Wapalestina, ndio maana wapiganaji wa muqawama wakaanzisha operesheni ya Kimbunga cha al-Aqsa na kuibua milingano mipya katika uwanja wa mapigano. Wamedhihirisha ukweli mpya katika medani ya vita, ukweli ambao hata majeshi ya nchi kadhaa yameshindwa kuufikia. Kwa makombora yake imara, muqawama umefanikiwa kuharibu pakubwa miundombinu ya Wazayuni na mifumo ya kijeshi ya utawala huo. Uungaji mkono wa umma kutoka Sri Lanka hadi Indonesia, Pakistan, Algeria, Iran, Iraq, Syria na nchi zote za Kiarabu na Kiislamu na wapigania uhuru wote katika mabara yote matano ya dunia pamoja na kubadilika misimamo rasmi ya baadhi ya serikali kwa maslahi ya taifa la Palestina na muqawama, huku Wazayuni wakiendelea kulaaniwa kimataifa kutokana na jinai zao dhidi ya Wapalestina wasio na hatia, yote hayo ni ishara tosha ya ushindi wa diplomasia ya muqawama wa Palestina pembeni ya shughuli za medani ya vita na ushindi wa kijeshi. Shughuli hizo zote bila shaka zinaharakisha ushindi wa mwisho wa kijeshi wa mapambano ya watu wa Palestina dhidi ya maghasibu wa Kizayuni. Ni lazima tujiandae kwa ajili ya vita hivyo vya ushindi kwa suhula zote tulizonazo na tufuatilie kuimarisha simulizi ya haki na uadilifu wa taifa la Palestina na kutoa usaidizi wote tulionao katika nyanja zote kwa ajili ya vita vya ukombozi ili ahadi ya Mwenyezi Mungu ipate kutimia."

Khalid al-Qadoumi

Kwa vyovyote vile, wapiganaji wa Palestina wamethibitisha kivitendo kwamba kamwe hawatatishwa na mipango ya kijeshi ya Wazayuni na uungaji mkono wa pande zote wa washirika wao wa jinai. Bila shaka sasa watawala wanaounga mkono mapatano wametambua kuwa tathmini yao kuhusu suala zima la Palestina na uwepo haramu wa Wazayuni si sahihi. Ni wazi kuwa operesheni ya Kimbunga cha al-Aqsa italeta mlingano mpya wa kisiasa na kijeshi katika eneo, hususan kuhusu suala zima la Palestina, ambapo kufuatia uungaji mkono mkubwa wa kieneo na kimataifa kwa operesheni hiyo, hali itaendelea kubadilika kwa manufaa ya Wapalestina na kutambuliwa rasmi ukombozi wa taifa la Palestina.