Jun 30, 2024 02:13 UTC
  • Kung'ang'ania vita bila ya malengo; jinai baada ya jinai nyingine

Vita vinaendelea huko Ukanda wa Gaza huku jeshi linalokalia kwa mabavu (Israel) likikabiliwa na ukosefu wa shabaha na kushambulia sehemu yoyote bila malengo.

Katika kipindi cha miezi 9 iliyopita, utawala wa Kizayuni umefanya mauaji makubwa mno huko Gaza. Umeendelea kufunga vivuko vyote na kuzuia kumika misaada ya chakula na misaada mingine mbalimbali katika ukanda huo mbali na kuligeuza eneo hilo kuwa magofu matupu.

Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Kuhudumia Watoto la Umoja wa Mataifa (UNICEF) amesema kwenye ripoti kwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kwamba miili ya maelfu ya watoto waliotoweka huko Gaza bado imefukiwa chini ya vifusi.

Kwa mujibu wa takwimu za Wizara ya Afya ya Palestina katika Ukanda wa Gaza, tangu kuanza vita hivyo hadi hivi sasa, zaidi ya watoto 15,600 wa Kipalestina wameshauawa shahidi na maelfu ya watoto waliojeruhiwa tangu tarehe 7 Oktoba mwaka jana 2023, wameongezeka na kufikia zaidi ya 37 watu elfu 765.

Hayo maandishi yaliyokoza ya gazeti la Javan yanawanukuu Wazayuni wakisema lazima waishambulie Gaza kwa bomu la nyuklia. 

Wizara ya Afya ya Palestina imetangaza kuwa; katika kipindi hicho, zaidi ya Wapalestina 86,429 wameshajeruhiwa kutokana na mashambulizi ya utawala wa Kizayuni. Kwa upande wake Shirika la Afya Duniani (WHO) limetaka maelfu ya Wapalestina waliojeruhiwa na wagonjwa wapelekwe nje ya Ukanda wa Gaza kwa matibabu la utawala wa Kizayuni unazuia.

Kwa mujibu wa WHO, tangu Oktoba 7 mwaka jana, watu 13,872 wameomba kuondoka Gaza kwa matibabu, lakini ni asilimia 35 tu kati yao wameondoka kwa msaada wa Shirika la Afya Duniani na washirika wake.

Takwimu za kijasusi za Marekani zinaonyesha kuwa iwapo utawala katili wa Israel utaendelea kukwamisha juhudi za kufikia makubaliano ya kusitisha vita kati yake na na Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina, Hamas, huenda kukatokea vita vikubwa kati ya Israel na Hizbullah. Wiki mbili zilizopita, Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lilipsasisha azimio la kuunga mkono usitishaji vita huko Gaza, lakini Benjamin Netanyahu, waziri mkuu katili wa utawala wa Kizayuni alikwamisha juhudi hizo kutokana na kung'ang'ania vita na mauaji ya Wapalestina huko Gaza.

Lakini hali halisi ilivyo baada ya takriban miezi 9 inaonyesha kushindwa mipango ya kijeshi ya utawala wa Kizayuni kaika Ukanda wa Gaza.

Kwa sababu Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina, Hamas imeweka mikakati ya kipekee ya kijeshi na inatumia mbinu ambazo zimesababisha kuchoka sana wanajeshi wa israel na akili zao nazo zimechoka.

Vile vile  utawala wa Kizayuni umeshindwa kufanikisha lengo lake hata moja sipokuwa jinai, mauaji, uharibifu, ukiukaji wa sheria za kimataifa, uripuaji wa mashirika ya misaada kibinadamu na kusababisha njaa kwa wakazi wa Palestina huko Ukanda wa Gaza.

Kasi ya kufikisha misaada ya kiutu ni ndogo, yaonya WHO

Utawala wa wa Kizayuni wa Israel umeshindwa katika vita hivyo, na hata baada ya kuiopita miezi 9, haujaweza kuyafanya makundi ya muqawama kama Hamas kusalimu amri katika eneo dogo ambalo imelizingira kila upande na licha ya kwamba utawala wa Kizayuni unaungwa mkono na madola yote ya kibeberu na vibaraka wao duniani, lakini imeshindwa kupata ushindi katika eneo dogo tu kama la Gaza na unaishia kufanya jinai za kutisha dhidi ya watoto wadogo, wanawake na vizee wasio na hatia.

Kushindwa jeshi la Kizayuni na baraza la vita la Netanyahu kufikia malengo waliyowatangazia walimwengu kuhusu vita vya Gaza, kumezidisha ukosoaji wa ndani na nje dhidi ya Netanyahu na kundi lake na ndio maana kila siku maandamano ya mamilioni ya walowezi wa Kizayuni yanafanyika ili kumshinikiza nduli huyo wa Israel ajiuzulu.