Wanahabari 5 ni miongoni mwa Wapalestina 29 waliouawa Gaza
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i113756-wanahabari_5_ni_miongoni_mwa_wapalestina_29_waliouawa_gaza
Wizara ya Afya ya Ukanda wa Gaza imesema waandishi wa habari watano ni miongoni mwa Wapalestina 29 waliouawa shahidi ndani ya saa 24 zilizopita na wanajeshi makatili wa Israel katika eneo hilo la Palestina linalokaliwa kwa mabavu na utawala wa Kizayuni.
(last modified 2024-07-06T07:50:41+00:00 )
Jul 06, 2024 07:50 UTC
  • Wanahabari 5 ni miongoni mwa Wapalestina 29 waliouawa Gaza

Wizara ya Afya ya Ukanda wa Gaza imesema waandishi wa habari watano ni miongoni mwa Wapalestina 29 waliouawa shahidi ndani ya saa 24 zilizopita na wanajeshi makatili wa Israel katika eneo hilo la Palestina linalokaliwa kwa mabavu na utawala wa Kizayuni.

Ofisi ya Habari ya Gaza imewataja wanahabari hao kuwa Amjad Jahjouh wa Shirika la Habari la Palestina;  Wafa Abu Dabaan wa Idhaa ya Chuo Kikuu cha Kiislamu Gaza, na Rizq Abu Ashkian wa Shirika la Habari la Palestina; waliouawa shahidi huko Nuseirat.

Waandishi wa habari wengine waliouawa shahidi huko Gaza ni Saadi Madoukh na Ahmed Sukkar wa Shirika la Habari la Deep Shot, waliouawa shahidi katika jiji la Gaza.

Takwimu rasmi zinasema kuwa, zaidi ya waandishi wa habari 155 wameshauawa shahidi katika Ukanda wa Gaza tangu utawala wa Kizayuni ulipoanzisha mashambulizi ya pande zote dhidi ya eneo hilo lililozingirwa Oktoba 7, 2023.

Wakati huo huo, Philippe Lazzarini, Mkurugenzi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi wa Kipalestina (UNRWA) amesema mwenendo wa utawala wa Kizayuni wa kuwafukuza Wapalestina kwenye makazi na mahema yao unapasa kukomeshwa.

Jinai zisizo na kikomo za Israel Nuseirat

Malaki ya wakimbizi wa Kipalestina sasa wanaishi barabarani baada ya kufukuzwa kwenye mahema yao mashariki mwa Khan Yunis, kusini mwa Ukanda wa Gaza.

Kwa mujibu wa Wizara ya Afya ya Ukanda wa Gaza, idadi ya Wapalestina waliouwa shahidi hadi hivi sasa tangu tarehe 7 Oktoba 2023 imepindukia watu 38,000 huku zaidi ya 87,000 wakijeruhiwa.

Wanamuqawama wa Palestina wakiongozwa na Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS hata hivyo wameendelea kukabiliana na jinai za kijeshi za utawala wa Kizayuni hususan katika mji wa Rafah wa kusini mwa Ukanda wa Gaza.