Sayyid Nasrullah: Magenge ya kigaidi yameundwa na Marekani na Uingereza
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i113968-sayyid_nasrullah_magenge_ya_kigaidi_yameundwa_na_marekani_na_uingereza
Katibu MKuu wa Hizbullah ya Lebanon amesema kuwa magenge ya kigaidi katika eneo la Asia Magharibi yameundwa na yanaendeshwa na mashirika ya kijasusi ya Marekani na Uingereza.
(last modified 2026-01-14T08:12:18+00:00 )
Jul 12, 2024 03:17 UTC
  • Sayyid Nasrullah: Magenge ya kigaidi yameundwa na Marekani na Uingereza

Katibu MKuu wa Hizbullah ya Lebanon amesema kuwa magenge ya kigaidi katika eneo la Asia Magharibi yameundwa na yanaendeshwa na mashirika ya kijasusi ya Marekani na Uingereza.

Shirika la habari la IRNA limeripoti habari hiyo leo Ijumaa na kumnukuu Sayyid Hassan Nasrullah akisema jana usiku katika mkesha wa siku ya sita ya mwezi mtukufu wa Muharram kwamba, mashirika ya kijasusi ya Marekani yameunda na yanaendesha magenge ya kigaidi kwa lengo la kuvunjia heshima itikadi tukufu za Kiislamu kama jihadi, kukubali kufa shahidi katika njia ya Allah na muqawama.

Katibu Mkuu huyo wa Hizbullah ya Lebanon ameongeza kuwa, mwaka 2000, maadui walifanya njama kubwa kwa kutumia mabanda yao ya propaganda, kueneza uongo kuhusu itikadi takatifu za Uislamu kama jihadi na muqawama ili kupotosha fikra za walimwengu.

Amesema, kwa mujibu wa mafundisho ya Qur'ani Tukufu, Mwenyezi Mungu amemwandalia mwanadamu maisha ya ufanisi na furaha, si Akhera tu, bali pia hapa duniani, hivyo magenge ya kigaidi hayana uhusiano wowote na Uislamu.