Muendelezo wa mashambulizi makali ya Hizbullah ya Lebanon kaskazini mwa Palestina inayokaliwa kwa mabavu (Israel)
(last modified 2024-10-12T11:41:25+00:00 )
Oct 12, 2024 11:41 UTC
  • Muendelezo wa mashambulizi makali  ya Hizbullah ya Lebanon  kaskazini mwa Palestina inayokaliwa kwa mabavu (Israel)

Harakati ya Muqawama ya Hizbullah ya Lebanon imelenga maeneo ya kaskazini mwa Palestina inayokaliwa kwa mabavu (Israel) kwa mashambulizi makali ya makombora.

Muqawama wa Kiislamu wa Lebanon umetangaza katika taarifa yake leo kuwa, kiwanda cha kuzalisha mada za  milipuko cha utawala wa Kizayuni kilichoko kusini mwa eneo la "Haifa" kaskazini mwa ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu na Israel  kimelengwa kwa mashambulizi makali  ya makombora.

Muqawama wa Kiislamu wa Lebanon ikiwa ni katika kuwaunga mkono watu wa Ukanda wa Gaza na Lebanon na wananchi wake, umeshambulia kwa makombora mkusanyiko wa wanajeshi  wa utawala wa Kizayuni katika kituo cha Al-Jardah, Zareit na kituo kingine cha jeshi la utawala wa Kizayuni katika eneo la "Mailya".

Wanamapambano wa Hizbullah, pia wamelenga buldoza la jeshi la utawala wa Israel katika kituo cha Ramya kwa makombora.

Tangu Septemba 23, jeshi la utawala habithi wa  Israel linaendesha mashambulizi makali  na ya kigaidi katika maeneo mbalimbali ya kusini mwa Lebanon na mji mkuu wa nchi hiyo Lebanon.
Hizbullah mbali na kuwalenga wanajeshi, imefanya oparesheni kadhaa dhidi ya maeneo na vitongoji vya walowezi wa Kizayuni katika Palestina inayokaliwa kwa mabavu na Israel  ambapo katika siku na saa zilizopita imerusha mamia ya makombora na kushambulia vituo vya kijeshi vya  utawala huo ghasibu wa Kizayuni.

Tags