Saudia na Uturuki zajiandaa kutuma vikosi vya nchi kavu Syria?
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i1183-saudia_na_uturuki_zajiandaa_kutuma_vikosi_vya_nchi_kavu_syria
Saudi Arabia na Uturuki zimesema kuwa huenda karibuni hivi zikaanzisha mashambulizi ya nchi kavu nchini Syria eti kwa lengo la kukabiliana na kundi la kigaidi na kitakfiri la Daesh!
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Feb 13, 2016 11:57 UTC
  • Saudia na Uturuki zajiandaa kutuma vikosi vya nchi kavu Syria?

Saudi Arabia na Uturuki zimesema kuwa huenda karibuni hivi zikaanzisha mashambulizi ya nchi kavu nchini Syria eti kwa lengo la kukabiliana na kundi la kigaidi na kitakfiri la Daesh!

Mevlut Cavusoglu, Waziri wa Mambo ya Nje wa Uturuki amesema Ankara na Riyadh zinajiadaa kwa operesheni ya ardhini nchini Syria na kwamba ndege za kivita za Saudia tayari zimeanza kuingia katika kambi ya Incirlik nchini Uturuki, ambayo kwa sasa inatumiwa na Marekani, Ufaransa na Uingereza katika hujuma zao ndani ya Syria.

Wakati huo huo, Shirika la Kijeshi la NATO linatafakari kuingia katika vita vinavyoendelea katika nchi za Syria na Iraq. Hayo yamedokezwa na Waziri wa Ulinzi wa Marekani, Ashton Carter ambaye amedai kuwa, NATO itaingia katika vita kwa lengo la kukabiliana na magaidi wa Daesh katika nchi hizo mbili.

Hayo yanajiri katika hali ambayo Alhamisi iliyopita Waziri Mkuu wa Russia, Dmitry Medvedev alionya kuwa iwapo vikosi vya kigeni vitavamia Syria basi huo utakuwa mwanzo wa vita vipya vikuu vya dunia. Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Syria Walid al Muallem naye ameonya kuwa askari wowote vamizi nchini Syria watarejea nyumbani kwao katika majeneza. Marekani na waitifaki wake wanaipinga vikali serikali halali ya Syria huku wakiunga mkono magaidi na wanamgambo wanaotaka kuipindua serikali ya Rais Bashar al Assad na wamechukua uamuzi wa kutuma majeshi ya nchi kavu nchini humo baada ya kuona magaidi hao wakielekea kushindwa kikamilifu.