Waisraeli waendelea kupinga hatua ya Netanyahu ya kumtimua Gallant
Miji mbalimbali ya Israel (Palestina inayokaliwa kwa mabavu) hususan Tel Aviv iimeendelea kushuhudia maandamano makubwa ya kupinga hatua ya Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu ya kumfuta kazi Waziri wa Vita wa utawala huo, Yoav Gallant.
Ripoti zinasema kuwa, maelfu ya Waisraeli wamefanya maandamano mjini Tel Aviv na miji mingine katika maeneo yanayokaliwa kwa mabavu na kkuitaka serikali ya utawala huo kuwarejesha nyumbani mateka wanaoshikiliwa Gaza.
Waandamanaji hao huku wakiimba nyimbo za kumpinga Netanyahu wamesisitiza kuwa, wanataka utawala huo ufikie makuabliano na Harakatii ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS ya kubadiilishana mateka na hivyo kuandaa mazingiira ya mateka 97 wanaoishikiliwa Gaza kurejea nyumbani.
Netanyahu na Gallant wamekuwa wakivutana mara kwa mara kuhusu operesheni ya mauaji ya kimbari ya utawala huo haramu dhidi ya Wapalestina huko Gaza.
Ofisi ya waziri mkuu wa Israel imesema kuwa, Netanyahu amemteua Waziri wa Mashauurii ya Kigeni wa utawala huo, Israel Katz kuchukua nafasi ya Gallant.
Hii ni katika hali ambayo, Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC), Karim Khan ameendelea kuwataka majaji wa mahakama hiyo watoe haraka waranti wa kukamatwa Netanyahu na Gallant.