Syria yatuma barua kwa Umoja wa Mataifa ikilaani mashambulizi ya Uturuki
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i1243-syria_yatuma_barua_kwa_umoja_wa_mataifa_ikilaani_mashambulizi_ya_uturuki
Wizara ya Mambo ya Nje ya Syria imetuma barua kwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa na kulaani mahambulizi ya ndege za kivita za Uturuki katika ardhi ya nchi hiyo.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Feb 14, 2016 10:29 UTC
  • Syria yatuma barua kwa Umoja wa Mataifa ikilaani mashambulizi ya Uturuki

Wizara ya Mambo ya Nje ya Syria imetuma barua kwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa na kulaani mahambulizi ya ndege za kivita za Uturuki katika ardhi ya nchi hiyo.

Wizara ya Mambo ya Nje ya Syria leo imetuma barua mbili kwa Mwenyekiti wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa na kwa Katibu Mkuu wa umoja huo na ikilaani mashambulizi ya ndege za Uturki katika ardhi ya nchi hiyo. Wizara ya Mambo ya Nje ya Syria imetangaza kuwa Uturuki imetekeleza mashambulizi hayo lengo likiwa ni kuyaunga mkono moja kwa moja makundi ya kigaidi na kupandisha ari ya makundi ya kigaidi yaliyoshindwa katika medani za mapambano.

Katika barua hizo, Wizara ya Mambo ya Nje ya Syria imeeleza kuwa matamshi ya Ahmad Daud Oghlo Waziri Mkuu wa Uturuki aliyesema kuwa upo udharura wa kuingilia kati huko Syria, ni kukiri rasmi Uturuki kukiuka maamizo ya Baraza la Usalama kuhusianana na mapambano dhidi ya ugaidi.

Barua mbili hizo zilizoandikwa na Wizara ya Mambo ya Nje ya Syria kwa Baraza la Usalama na Umoja wa Mataifa zimeendelea kueleza kuwa serikali ya nchi hiyo inalaani jinai na mashambulizi ya mara kwa mara ya Uturuki katika ardhi ya Syria na kulitaka Baraza la Usalama kutekeleza majukumu yake ya kulinda amani na usalama wa kimataifa na kuzuia jinai za utawala wa Uturuki.