Zaidi ya magaidi 1000 wa Daesh waangamizwa mkoani al-Anbar, Iraq
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i14221-zaidi_ya_magaidi_1000_wa_daesh_waangamizwa_mkoani_al_anbar_iraq
Mamia ya wapiganaji wa kundi la kigaidi na kitakfiri la Daesh wameangamizwa katika operesheni za kulisafisha eneo la al-Khalidiyyah mkoania al-Anbar nchini Iraq.
(last modified 2023-11-27T12:14:11+00:00 )
Aug 30, 2016 04:00 UTC
  • Zaidi ya magaidi 1000 wa Daesh waangamizwa mkoani al-Anbar, Iraq

Mamia ya wapiganaji wa kundi la kigaidi na kitakfiri la Daesh wameangamizwa katika operesheni za kulisafisha eneo la al-Khalidiyyah mkoania al-Anbar nchini Iraq.

Hadi al-Amiri, Katibu wa Taasisi ya Badr nchini Iraq ametangaza kuwa, katika operesheni za kukisafisha kisiwa cha al-Khalidiyyah kilichokuwa kinakaliwa na wanachama wa genge hilo la ukufurishaji la Daesh mkoani al-Anbar, zaidi ya magaidi 1000 wameangamizwa. Kwa mujibu wa ripoti hiyo, katika operesheni hizo, harakati ya wananchi ya kujitolea ya Hashd al-Shaab imewatia mbaroni pia makumi ya magaidi wa kundi hilo. Habari nyingine zinaeleza kuwa harakati ya wananchi imefanikiwa kuharibu ndege moja isiyo na rubani iliyokuwa inamilikiwa na wanachama wa Daesh katika mji wa Bayji, ulioko mkoani Saladin, kaskazini mwa nchi hiyo.

Jeshi la Iraq likifurahia ushindi dhidi ya magaidi wa Daesh

Tangu mwezi mmoja uliopita sanjari na operesheni za kuukomboa mji wa Fallujah kutoka mikononi mwa wanachama wa Daesh, jeshi la Iraq limekuwa likitekeleza operesheni kadhaa kaskazini mwa nchi hiyo na katika mkoa wa Saladin, ambapo hadi sasa limefanikiwa kudhibiti makumi ya vijiji na maeneo muhimu ya kusini mwa mji wa Mosul kutoka mikononi mwa magaidi hao. Wakati huo huo duru za habari mjini Mosul zimearifu kwamba, kundi la kigaidi na kitakfiri la Daesh limepunguza idadi ya wapiganaji wake mjini hapo kwa zaidi ya asilimia 70. Kwa mujibu wa habari hiyo, kundi hilo limepunguza wapiganaji wake kutoka elfu 12 na kufikia elfu tatu na kwamba hali hiyo imetokana na uhaba mkubwa wa wanachama wake.