Magaidi 40 waangamizwa katika mashambulio ya anga Halab Syria
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i15712-magaidi_40_waangamizwa_katika_mashambulio_ya_anga_halab_syria
Vikosi vya Syria vikisaidiwa na ndege za kijeshi za Russia vimefanikiwa kuwaangamiza magaidi 40 katika mji wa Halab ambao ni wanachama wa kundi la kigaidi la Jabhat al-Nusra.
(last modified 2026-01-14T08:12:18+00:00 )
Sep 20, 2016 09:12 UTC
  • Magaidi 40 waangamizwa katika mashambulio ya anga Halab Syria

Vikosi vya Syria vikisaidiwa na ndege za kijeshi za Russia vimefanikiwa kuwaangamiza magaidi 40 katika mji wa Halab ambao ni wanachama wa kundi la kigaidi la Jabhat al-Nusra.

Wizara ya Ulinzi ya Russia imeripoti kwamba, ndege za kijeshi za nchi hiyo leo zikivisaidia vikosi vya Syria zimewauawa magaidi 40 kaskazini mwa mji wa Halab.

Kufuatia mashambulio hayo, magaidi hao wameondoka katika baadhi ya maeneo waliyokuwa wakiyadhibiti na hivyo jeshi la Syria kuyadhibiti maeneo hayo.

Taarifa zaidi zinasema kuwa, vifaa na zana nyingi za kijeshi za magaidi hao wa Jabhat al-Nusran yakiwemo magari 11 zyameteketezwa katika mashambulio hayo.

Magaidi wa Daesh walivyoangamizwa na jeshi la Syria

Wakati huo huo, jeshi la Syria kwa kushirikiana na wanamapambano limeendelea kusonga mbele katika maeneo yaliyokuwa yakidhibitiwa na wanachama wa makundi ya kigaidi na kitakfiri.

Kwa mujibu wa ripoti mbalimbali ni kuwa, makundi ya kigaidi yanayoungwa mkono na Marekani, Uturuki, utawala haramu wa Israel na baadhi ya nchi Kiarabu yameendelea kupata pigo na kupoteza maeneo mengi ambayo walikuwa wakiyadhibiti.

Ikumbwe kuwa, hivi karibuni Rais Bashar al-Assad alisema kuwa, kila Syria inapopata ushindi mkubwa katika medani za vita au mazungumzo ya kitaifa ya amani, nchi zinazoipinga serikali ya nchi hiyo  zinazidisha misaada na uungaji mkono wao kwa makundi ya kigaidi; hata hivyo kusimama kidete taifa hilo kumekwamisha njama zote za maadui.