Feb 21, 2016 16:13 UTC
  • Makumi wauawa katika miripuko ya mabomu Syria

Kwa akali watu 30 wamethibitishwa kuuawa na wengine wengi kujeruhiwa katika wimbi la miripuko ya mabomu lililotikisa viunga vya mji mkuu Damascus na Homs nchini Syria.

Habari zinasema kuwa, miripuko hiyo iliyiotokea leo Jumapili imetokea katika wilaya ya Sayeda Zeinab, karibu na Haram ya Bibi Zeinab SA, mjukuu wa Mtume Mtukufu SAW. Habari zinasema kuwa, miripuko iliyotokea ni minne ikiwemo miwili ilioyolenga magari katika barabara ya al-Tin. Hata hivyo hakuna kundi lolote lililotangaza kuhusika na shambulio hilo la kigaidi, lakini kidole cha lawama kinaelekezewa kundi la kigaidi na kitakfiri la Daesh ambalo limekuwa likifanya mashambulio ya aina hiyo nchini Syria na Iraq. Miripuko hiyo imetokea masaa machache baada ya kutokea mashambulizi mengine mawili katika mkoa wa Homs, magharibi mwa Syria, ambapo watu zaidi 57 wameripotiwa kuuawa na wengine zaidi ya 100 wakijeruhiwa. Waziri Mkuu wa Syria Wael al-Halqi amelaani mashambulizi hayo dhidi ya raia wasio na hatia na kusisitiza kuwa, taifa la Syria litaendelea kusimama kidete kupambana na ugaidi. Hii ni katika hali ambayo, Waziri wa Mambo ya Nje wa Saudi Arabia ametaka magaidi walioko nchini Syria waimarishwe kwa silaha. Adel al-Jubeir amesema hayo katika mahojiano aliyofanyiwa na gazeti la Kijerumani la Der Spiegel na kutamka waziwazi bila ya kificho kuwa makundi yanayobeba silaha (akikusudia magenge ya kigaidi) lazima yapatiwe makombora ya kutungulia ndege. Al-Jubeir ameongeza kijeuri kuwa, endapo magenge hayo yatakuwa na silaha za kisasa, yataweza kuipindua serikali ya Syria.

Tags