Wasyria waandamana kuunga mkono harakati ya Hizbullah
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i2596-wasyria_waandamana_kuunga_mkono_harakati_ya_hizbullah
Raia wa maeneo kadhaa ya Syria wamefanya maandamano wakitangaza uungaji mkono wao kwa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Hizbullah ya nchini Lebanon.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Mar 07, 2016 03:38 UTC
  • Wasyria waandamana kuunga mkono harakati ya Hizbullah

Raia wa maeneo kadhaa ya Syria wamefanya maandamano wakitangaza uungaji mkono wao kwa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Hizbullah ya nchini Lebanon.

Wakazi wa miji ya Al-Fu'ah na Kufriya kaskazini mwa jimbo la Idlib nchini Syria na ambao wamekuwa wakizingirwa na makundi ya kigaidi kwa muda mrefu sasa, walifanya maandamano hayo hapo jana, ambapo sanjari na kulaani hatua za Baraza la Ghuba ya Uajemi za kuitaja harakati ya Hizbullah kuwa ya kigaidi, wameunga mkono pia nafasi ya harakati hiyo ya Kiislamu katika kupambana na maadui wa Uislamu ikiwemo Israel na makundi ya kigaidi. Waandamanaji hao sanjari na kutoa nara za kuunga mkono nafasi chanya ya kimapambano ya Hizbullah katika kukabiliana na utawala haramu wa Kizayuni na kuwatetea watu wanaodhulumiwa wa Palestina na kadhalika mapambano yake dhidi ya wanachama wa makundi ya kigaidi na kitakfiri yanayotumikia maslahi ya Marekani na utawala wa Kizayuni, wamesisitiza udharura wa kuongezwa juhudi zaidi za kujitolea za harakati hiyo ya Hizbullah. Jumatano iliyopita, Baraza la Ushirikiano la Ghuba ya Uajemi linaloundwa na nchi za Saudia, Oman, Bahrain, Kuwait, Qatar na Imarat liliweka harakati ya Hizbullah katika orodha ya makundi ya kigaidi, hatua ambayo mbali na kukosolewa vikali na pande mbalimbali, imetajwa kuwa imechukuliwa kufuatia mashinikizo ya serikali ya Washington na utawala wa Kizayuni. Mbali na Syria, nchi za Lebanon, Iraq, Algeria na Tunisia zimepinga vikali hatua hiyo ya PGCC na kutangaza wazi kuwa hazitoheshimu maamuzi ya baraza hilo kuihusu harakati hiyo ya Kiislamu.