Answarullah yashambulia kwa kombora uwanja wa ndege wa Jazan, Saudia
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i39095-answarullah_yashambulia_kwa_kombora_uwanja_wa_ndege_wa_jazan_saudia
Jeshi la Yemen kwa kushirikiana na harakati ya wananchi ya Answarullah, limeushambulia kwa kombora uwanja wa ndege wa Jazan, kusini magharibi mwa Saudia ikiwa ni katika hatua ya ulipizaji kisasi kutokana na uvamizi wa Saudia na washirika wake dhidi ya taifa hilo la Kiarabu.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jan 17, 2018 04:47 UTC
  • Answarullah yashambulia kwa kombora uwanja wa ndege wa Jazan, Saudia

Jeshi la Yemen kwa kushirikiana na harakati ya wananchi ya Answarullah, limeushambulia kwa kombora uwanja wa ndege wa Jazan, kusini magharibi mwa Saudia ikiwa ni katika hatua ya ulipizaji kisasi kutokana na uvamizi wa Saudia na washirika wake dhidi ya taifa hilo la Kiarabu.

Hata hivyo kanali ya televisheni ya al-Masira ya Yemen haikuweka wazi kiwango cha uharibifu uliotokana na shambulizi hilo. Jeshi la Yemen limetoa taarifa hiyo katika hali ambayo siku chache zilizopita Sharaf Luqman, msemaji wa Jeshi hio alitangaza habari ya kubadilishwa mfumo wa vita dhidi ya taifa vamizi la Saudia katika siku chache zijazo.

Harakati ya wananchi ya Answarullah nchini Yemen

Aidha siku chache zilizopita kikosi cha mizinga cha jeshi la Yemen na harakati hiyo ya wananchi walifanikiwa kutungua ndege mbili za kivita za Saudia kwa kutumia makombora ya ardhi kwa anga. Uwezo wa kujilinda wa jeshi la Yemen na harakati ya Answarullah unajiri katika hali ambayo taifa hilo limezingirwa na Saudia na washirika wake wa Marekani, Israel na baadhi ya nchi za Kkiarabu kila upande kuanzia nchi kavu, anga na baharini tangu mwezi Machi mwaka 2015. Licha ya Saudia kuungwa mkono na madola hayo lakini imeshindwa kufikia malengo yake machafu ghairi ya kusababisha maafa na uharibifu wa miundombinu dhidi ya taifa hilo masikini la Kiarabu.