Ufyatuaji risasi katika kituo cha gadi ya kitaifa ya Saudi Arabia
(last modified Thu, 31 May 2018 11:27:06 GMT )
May 31, 2018 11:27 UTC
  • Ufyatuaji risasi katika kituo cha gadi ya kitaifa ya Saudi Arabia

Vyonzo vya habari vimetangaza kutokea ufyatuaji risasi katika mji wa Taif ulioko magharibi mwa Saudia Arabia. Ripoti zinasema kuwa watu wawili waliokuwa na silaha waliingia katika kituo cha gadi ya kitaifa kilichoko mjini hapo, baada ya kumshambulia askari usalama mmoja katika eneo hilo.

Katika miezi ya hivi karibuni kumetokea matukio ya utumiaji silaha moto katika baadhi ya miji mikubwa ya Saudi Arabia ukiwemo mji mkuu Riyadh, jambo ambalo linaonyesha wazi kwamba watawala wa nchi hiyo wameshindwa kulinda usalama nchini humo. Hatua ya serikali ya Saudia ya kutekeleza siasa kali za kudhibiti uchumi zikiwemo za kuongeza bei ya bidhaa za msingi na kodi ya malipo, imewaongezea mashinikizo makubwa ya kiuchumi raia wa kawaida kwa upande mmoja, na umuzi wa Muhammad bin Salman, Mrithi wa Kiti cha Ufalme wa Saudia wa kuwatia mbaroni makumi ya wanawafalme wenzake umewakasirisha sana wanawafalme hao na kuwafanya watake kulipiza kisasi, kwa upande wa pili.

Mfalme Salman akiwa na mwanae, Muhammad bin Salman

Mwezi Aprili uliopita, Riyadh ilikuwa uwanja wa mapigano ya masaa kadhaa kati ya watu wasiojulikana na askari usalama wa Saudia. Gazeti la Rai al-Yaum liliandika kuhusu suala hilo kwamba Wasaudia wengi wanaamini kuwa tukio hilo la ufyatulianaji risasi katika kasri ya mfalme mjini Riyadh lilitokana na  hitilafu za ndani ya ukoo unaotawala nchi hiyo. Tokea wakati huo Muhammd bin Salman hajaonekana hadhari kwa muda wa mwezi mmoja jambo ambalo limeongeza dhana kwamba huenda alijeruhiwa katika tukio hilo. Kutokuwepo uwazi miongoni mwa watawala wa Saudia katika uwanja huo kumezidisha uvumi juu ya suala hilo. Pamoja na hayo, jambo la kuzingatiwa hapa ni kukaririwa matukio ya kiusalama katika pembe togfauti za nchi hiyo ambako kunathibitisha wazi kuwa watawala hao wameshindwa kulinda usalama nchini. Maudhui hiyo inabainisha wazi kushindwa watawala wa ukoo wa Aal Saud kuongoza nchi katika nyanja tofauti na hasa za kiusalama.

Baadhi ya wanawafalme wa Saudia waliotiwa mbaroni na Muhammad bin Salman

Watawala hao kwa sasa wanakabiliwa na changamoto mbili muhimu. Ya kwanza ni jinsi ya kukabidhi madaraka kwa kizazi kipya. Tokea wakati wa kubuniwa ufalme wa Saudia, ufalme huo umekuwa ukizunguka miongoni mwa watoto wa Abdul Aziz, mwanzilishi wa ufalme huo. Lakini mfalme wa hivi sasa, Salman bin Abdul Aziz amekiuka utaratibu huo na kumchagua mwanwe kuwa mrithi wa kiti cha ufalme, jambo ambalo limewakasirisha sana wanwafalme wengine wa nchi hiyo. Kwa hatua yake hiyo, Salman amegeuza utaratibu wa kuteuliwa wafalme wa nchi hiyo kutoka mfumo wa ndugu kwa ndugu na kuwa wa baba kwa mwana. Wanawafalme wengine wamekasirishwa na jambo hilo kwa sababu linafanya familia moja tu kuhodhi madaraka. Wanalichukulia suala hilo kuwa aina fulani ya mapinduzi kwa sababu limekiuka misingi yote ya taratibu zilizowekwa za kuteuliwa mfalme na hivyo litakuwa na matokeo mabaya kwa utawala wa nchi hiyo katika siku zijazo, ambapo tayari tumeanza kuona athari zake katika baadhi ya sehemu za nchi hiyo.

Uhusiano wa karibu wa watawala wa Saudia na Wamagharibi wanaopiga vita Uislamu

Changamoto ya pili inahusiana na masuala ya kisiasa, kijamii na kiuchumi. Mabadiliko ya kisiasa, kijamii na kiuchumi yanapasa kufanyika taratibu lakini haijakuwa hivyo nchini Saudia. Mabadiliko ambayo yamekuwa yakifanywa na Muhammad bin Salman katika nyanja hizo na kuandamana na kutiwa mbaroni wanawafalme wengine, yamezua malalamiko na upinzani mkubwa dhidi yake. Ni kutokana na ukweli huo ndipo familia ya Bin Salman ikawa inasubiri kutokea radiamali na mapinduzi wakati dhidi yake wowote. Kwa msingi huo familia hiyo inaiishi katika hali ya  jinamizi na woga mkubwa. matukio ya Saudia bila shaka yanathibitisha kwamba ukoo wa kifalme wa Aal Saud unaishi katika mazingira magumu na ya kulegalega katika kipindi hiki cha utawala wa Salman bin Abdul Aziz.