Hizbullah: Mipango yote ya Marekani, Israel na Saudia itafeli
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i45954-hizbullah_mipango_yote_ya_marekani_israel_na_saudia_itafeli
Mjumbe wa Baraza Kuu la harakati ya Hizbullah ya Lebanon, Nabil Qaouk amesema kuwa, mipango ya pamoja ya Marekani, utawala haramu wa Israel na Saudi Arabia itaishia kushindwa.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jun 16, 2018 21:03 UTC
  • Hizbullah: Mipango yote ya Marekani, Israel na Saudia itafeli

Mjumbe wa Baraza Kuu la harakati ya Hizbullah ya Lebanon, Nabil Qaouk amesema kuwa, mipango ya pamoja ya Marekani, utawala haramu wa Israel na Saudi Arabia itaishia kushindwa.

Sheikh Nabil Qaouk amefafanua kuwa, utawala wa Aal-Saud umeigeuza idi ya Waislamu wa Yemen kuwa mauaji na umwagaji damu mkubwa. Amesema kuwa uingiliaji wa Saudia katika masuala ya ndani ya Yemen kwa kisingizio cha kutaka kumrejesha madarakani Abdrabbuh Mansur Hadi, rais wa zamani na kibaraka wa Riyadh aliyejiuzulu nafasi hiyo na kutoroka nchi mwezi Machi 2015, umesababisha mauaji ya makumi ya maelfu ya watu na maelfu ya wengine kujeruhiwa sambamba na kuifanya Yemen iishiwe kabisa na chakula, madawa, na kuenea kwa maradhi ya kuambukiza. 

Bendera tatu maadui wakubwa wa watu wa Yemen

Mjumbe wa Baraza Kuu la harakati ya Hizbullah ameendelea kubainisha kwamba, siasa zote za Saudia na washirika wake yaani Marekani na Israel zimejengeka juu ya msingi wa kufanya njama dhidi ya mataifa ya eneo la Mashariki ya Kati hususan taifa madhlumu la Palestina. Saudia, Marekani, Israel na baadhi ya nchi za Kiarabu na bila kuzingatia jinai za utawala wa Kizayuni dhidi ya raia wa Palestina, zinashiriki katika njama ya kutekelezwa mpango uliopendekezwa na Washington wa 'Muamala wa Karne' wenye lengo la kuifuta kadhia ya Palestina kwa kuikabidhi Israel mji wa Quds na matukufu yake.