Hizbullah: Maandamano ya Wairaqi ni dhihirisho wanapinga uvamizi wa Marekani
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i58734-hizbullah_maandamano_ya_wairaqi_ni_dhihirisho_wanapinga_uvamizi_wa_marekani
Harakati ya Muaqawama ya Hizbullah ya Lebanon imewapongeza wananchi wa Iraq kwa kujitokeza kwa wingi katika maandamano ya kupinga uwepo wa askari wa Marekani katika nchi hiyo ya Kiarabu.
(last modified 2026-02-18T07:37:01+00:00 )
Jan 25, 2020 08:22 UTC
  • Hizbullah: Maandamano ya Wairaqi ni dhihirisho wanapinga uvamizi wa Marekani

Harakati ya Muaqawama ya Hizbullah ya Lebanon imewapongeza wananchi wa Iraq kwa kujitokeza kwa wingi katika maandamano ya kupinga uwepo wa askari wa Marekani katika nchi hiyo ya Kiarabu.

Katika taarifa, Hizbullah imesema, "wananchi wa Iraq wamethibitisha kuwa hawataki kabisa kuwepo wanajeshi wa Marekani katika ardhi ya nchi hiyo. Mkusanyiko huu mkubwa mtukufu unaonyesha umoja wa wananchi wa Iraq mkabala wa uvamizi wa Marekani na ubeberu."

Taarifa hiyo imebainisha kuwa, kujitokeza kwa mamilioni ya Wairaqi katika maandamano ya jana Ijumaa ni taswira halisi ya msimamo wa umma wa Kiarabu na Kiislamu dhidi ya Wamarekani.

Harakati ya Muaqawama ya Hizbullah ya Lebanon imesisitiza kuwa, maandamano ya jana ni ujumbe wa wazi kwa Washington kuwa wananchi wa Iraq wamechoshwa na namna Marekani inavyofonza rasilimali zao.

Wanachama wa Hizbullah ya Iraq

Wakati huohuo, Dhaifallah al-Shami Waziri wa Habari wa Yemen ameyataja maandamano hayo kama tukio la kihistoria na hatua moja ya kuanza kutimuliwa majeshi ya Marekani katika eneo la Asia Magharibi.

Amesema Yemen imedhihirisha mara kadhaa kuwa maandamano makubwa yanaweza kuupigisha magoti ubeberu wa Marekani katika eneo.