Feb 20, 2020 04:24 UTC
  • Seneta Sanders: Viongozi wa Saudi Arabia ni 'wauaji na majambazi'

Seneta wa Marekani, Bernie Sanders anayeongoza katika kinyang'anyiro cha kuwania tiketi ya chama cha Domocratic kwa ajili ya kugombea kiti cha rais wa nchi hiyo ameikosoa Saudi Arabia katika kampeni zake huko Las Vegas na kuwaita viongozi wa nchi hiyo kuwa ni 'wauaji na majambazi'.

Seneta huyo wa Vermint amemtaja mrithi wa ufalme wa Saudia, Muhammad bin Salman kuwa ni 'bilionea dikteta'. Amesisitiza kuwa hana tatizo na raia wa Saudi Arabia lakini nukta muhimu zaidi ni kwamba, nchi hiyo inaongozwa na wauaji majambazi.

Vilevile ameitaka serikali ya Marekani iache kupuuza mahitaji ya Wapalestina na kukosoa msimamo wa serikali ya kibaguzi ya mrengo wa kulia inayotawala sasa huko Israel.

Bernie Sanders

Seneta huyo wa Marekani ameashiria pia mgogoro wa kibinadamu wa wakazi wa eneo la Ukanda wa Gaza huko Palestina.

Disemba mwaka jana pia Bernie Sanders alitoa matamshi kama haya katika mjadala wa uchaguzi wa rais wa Marekani na kumtaja Waziri Mkuu wa utawala wa Kizayuni wa Israel, Benjamin Netanyahu kuwa ni mbaguzi. Alisema siasa za nje za Marekani hazipaswi kuendelea kuipendelea Israel bali pia inapaswa kuwajali Wapalestina.     

Tags