Meli ya mizigo ya Imarati yatia nanga katika bandari ya Israel
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i63990-meli_ya_mizigo_ya_imarati_yatia_nanga_katika_bandari_ya_israel
Meli ya mizigo ya Umoja wa Falme za Kiarabu imetia nanga katika mji wa bandari wa Haifa, katika maeneo ya Wapaestina yanayokaliwa kwka mabavu na utawala wa Kizayuni wa Israel.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Oct 13, 2020 04:31 UTC
  • Meli ya mizigo ya Imarati yatia nanga katika bandari ya Israel

Meli ya mizigo ya Umoja wa Falme za Kiarabu imetia nanga katika mji wa bandari wa Haifa, katika maeneo ya Wapaestina yanayokaliwa kwka mabavu na utawala wa Kizayuni wa Israel.

Kutia nanga kwa meli hiyo mjini Haifa, kunaashiria kuanza kwa safari za baharini za moja kwa moja baina ya Imarati na Israel. 

Eshel Armony, Mwenyekiti wa Bodi ya Bandari ya Haifa amethibitisha habari hiyo na kusema huenda usafirishaji huo wa mizigo kwa njia ya bahari baina ya tawala mbili hizo ukaongezeka hata zaidi katika siku za usoni.

Benjamin Netanyahu, Waziri Mkuu wa utawala haramu wa Israel jana Jumatatu aliliambia bunge la utawala huo pandikizi kuwa, kufanya biashara na UAE ni mwanzo wa mambo makubwa yanayokuja. Amesema, "leo (jana) meli ya mizigo imewasili kutoka Dubai ikiwa na mizigo. Mizigo ambayo ni bei rahisi sana itakayofaidi Waisraeli."

Ndege ya Israel ikitua katika uwanja wa ndege wa Abu Dhabi, nchini Imarati

Haya yanajiri chini ya mwezi mmoja baada ya kufanyika safari ya kwanza ya ndege ya moja kwa moja kati ya Uwanja wa Ndege wa Ben Gurion mjini Tel Aviv na Abu Dhabi nchini Imarati.

Katikati ya mwezi uliopita, Imarati na Bahrain zilisaini rasmi mapatano ya kuanzisha uhusiano wa kidiplomasia na utawala wa Kizayuni katika Ikulu ya White House nchini Marekani. Waislamu na wapenda haki kote duniani wameendelea kulaani usaliti huo wa UAE na Bahrain na kubainisha kuwa, hatua hiyo ni sawa na kuwachoma jambia kwa nyuma wananchi madhulumu wa Palestina.