Katika hatua ambayo haijawahi kushuhudiwa, Pompeo kutembelea vitongoji vya walowezi
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i64595-katika_hatua_ambayo_haijawahi_kushuhudiwa_pompeo_kutembelea_vitongoji_vya_walowezi
Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani amepanga kutembelea vitongoji vya walowezi wa Kizayuni katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu na utawala wa Kizayuni wa Israel ili kuhalalisha jinai za utawala huo haramu.
(last modified 2026-03-03T12:46:59+00:00 )
Nov 13, 2020 03:56 UTC
  • Katika hatua ambayo haijawahi kushuhudiwa, Pompeo kutembelea vitongoji vya walowezi

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani amepanga kutembelea vitongoji vya walowezi wa Kizayuni katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu na utawala wa Kizayuni wa Israel ili kuhalalisha jinai za utawala huo haramu.

Tovuti ya habari ya Axius imeripoti kuwa, katika hatua ambayo haijawahi kushuhudiwa, waziri wa mambo ya nje wa Marekani Mike Pompeo amepanga kutembelea vitongoji vya walowezi wa Kizayuni katika Ufukwe wa Magharibi wa Mto Jordan, Palestina inayokaliwa kwa mabavu na Miinuko ya Golan ya Syria.

Hii ikiwa na maana kwamba, Pompeo atakuwa waziri wa kwanza wa mambo ya nje wa Marekani kukiuka sheria za kimataifa kwa kutembelea vitongoji vya walowezi wa Kizayuni katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu.

Pompeo amedhamiria kufanya hivyo wakati tangu mwaka 1967, serikali zote za Marekani zimekuwa zikiitambua miinuko ya Golan ya Syria na vitongoji vya walowezi wa Kizayuni katika Ufukwe wa Magharibi wa Mto Jordan kuwa ni ardhi zinazokaliwa kwa mabavu na Israel.

Vitongoji vya walowezi wa Kizayuni katika ardhi za Palestina

Itakumbukwa kuwa mwezi Novemba 2019 wizara ya mambo ya nje ya Marekani ilibatilisha sera za nchi hiyo kuhusiana na ujenzi haramu wa vitongoji vya walowezi wa Kizayuni katika Ufukwe wa Magharibi zilizokuwa zimeratibiwa kuendana na sheria za kimataifa. 

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani leo anatazamiwa kuelekea Paris, Ufaransa kabla ya kuendelea na safari yake kuelekea Uturuki, Georgia, Palestina inayokaliwa kwa mabavu (Israel), Imarati, Qatar na Saudi Arabia.

Kinyume na ilivyoelezwa katika maazimio ya Umoja wa Mataifa, rais Donald Trump wa Marekani na serikali yake wameunga mkono hatua haramu na inayohalifu sheria ya utawala wa Kizayuni wa Israel ya kujenga vitongoji vya walowezi katika ardhi unazozikalia kwa mabavu.../