HAMAS yawahutubu Wazayuni: Mapambano ya Quds ni mapambano yetu sote
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i69462-hamas_yawahutubu_wazayuni_mapambano_ya_quds_ni_mapambano_yetu_sote
Mkuu wa ofisi ya kisiasa ya Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina HAMAS amesisitiza kuwa, ikiwa utawala haramu wa Kizayuni wa Israel utaendeleza siasa zake za kiuadui dhidi ya Quds hakutakuwapo na utulivu wowote.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Apr 26, 2021 03:29 UTC
  • HAMAS yawahutubu Wazayuni: Mapambano ya Quds ni mapambano yetu sote

Mkuu wa ofisi ya kisiasa ya Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina HAMAS amesisitiza kuwa, ikiwa utawala haramu wa Kizayuni wa Israel utaendeleza siasa zake za kiuadui dhidi ya Quds hakutakuwapo na utulivu wowote.

Ismail Haniya ametoa kauli hiyo sambamba na kusisitiza kuwa, matukio na machafuko ya hivi karibuni katika mji wa Baitul Muqaddas (Jerusalem) unaokaliwa kwa mabavu ni mapigano ya utambulisho wa mji huo na akaongeza kwamba, matukio ya Quds yamevunja na kuporomosha dhana ya kuanzisha uhusiano wa kawaida na adui Mzayuni, mpango uitwao Muamala wa Karne na pia dhana ya kukumbatia mazungumzo.

Haniya amekumbusha kuwa, Quds si ya Wapalestina peke yao, bali ni mhimili mkuu wa mapambano; na akayataka mataifa yote ya Kiarabu na Kiislamu yajiandae kutoa msaada wa dhati kwa taifa la Palestina na yaitumie stratejia ya kuunga mkono Quds kwa ajili ya kufanikisha mkakati wa kuihami na hatimaye kuikomboa Quds kikamilifu.

Askari katili wa utawala dhalimu wa Israel wakiwafyatulia mabomu ya kutoa machozi Wapalestina

Kwa muda wa siku kadhaa sasa, mji wa Baitul Muqaddas unaokaliwa kwa mabavu na baadhi ya miji mingine ya Palestina, inashuhudia mapigano kati ya askari wa utawala haramu wa Kizayuni wa Israel na waandamanaji na waumini Wapalestina wanaolalamikia jinai za utawala huo ghasibu dhidi ya msikiti wa Al Aqsa na Wapalestina.

Mkuu wa ofisi ya kisiasa ya Hamas amezungumzia pia uchaguzi wa Palestina na kubainisha kuwa, kusudio la Hamas la kushiriki uchaguzi limezingatia taswira pana na kamili ya mustakabali; na uchaguzi katika Quds tukufu inapasa uwe ni wa mapambano ya kitaifa.

Uchaguzi wa Bunge la Palestina umepangwa kufanyika tarehe 22 Mei, wa Rais wa Mamlaka ya Ndani tarehe 31 Julai na ule wa Baraza la Taifa la Palestina Agosti 31 mwaka huu.../