Israel yashindwa kuficha woga wake wa kukurubiana nchi za Waislamu
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i71828-israel_yashindwa_kuficha_woga_wake_wa_kukurubiana_nchi_za_waislamu
Rais wa utawala wa Kizayuni ameshindwa kuficha wahka na woga wake kutokana na kuwepo uwezekano wa nchi za Kiarabu kuelekea zaidi upande wa Iran.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jun 30, 2021 01:49 UTC
  • Israel yashindwa kuficha woga wake wa kukurubiana nchi za Waislamu

Rais wa utawala wa Kizayuni ameshindwa kuficha wahka na woga wake kutokana na kuwepo uwezekano wa nchi za Kiarabu kuelekea zaidi upande wa Iran.

Gazeti la Haaretz la utawala wa Kizayuni limezinukuu duru za kidiplomasia zikisema kuwa, rais wa Israel, Reuven Rivlin ameonesha kuhofishwa sana na hatua za kidiplomasia za Iran za kuimarisha uhusiano wake na nchi za Kiarabu za Ghuba ya Uajemi na kumlilia rais wa Marekani kuhusu jambo hilo.

Kwa mujibu wa gazeti hilo, Rivlin amemwambia Joe Biden kwamba kubadilika siasa za Washington kuhusu eneo la Asia Magharibi kutazifanya nchi za Kiarabu zijikurubishe zaidi kwa Iran.

Kwa upande wake, Joe Biden amewaambia Wazayuni wakati wa mazungumzo yake na rais wa utawala wa Kizayuni kwamba, wakati wa utawala wake, atahakikisha kuwa Iran haimiliki kile alichodai eti silaha za nyuklia. 

Rais wa Marekani, Joe Biden

 

Ikumbukwe kuwa kipindi cha miaka saba cha urais wa Reuven Rivlin huko israel kinamalizika tarehe 9 mwezi Julai yaani baada ya wiki moja na kitu. 

Wazayuni wanaendelea kutoa madai kama hayo katika hali ambayo utawala wa Kizayuni wa Israel ndio utawala pekee unaomiliki silaha angamizi za nyuklia katika eneo zima la Asia Magharibi. Viwanda vya utawala huo pandikizi vimejaa silaha hizo haramu na hatari mno kwa usalama wa eneo hili na dunia nzima kwa ujumla.

Cha kushangaza ni kuwa si Umoja wa Mataifa, si madola ya Magharibi, si wakala wa kimataifa wa IAEA na si mashirika yanayotetea haki za binadamu yanayochukua hatua za kuuzuia utawala wa Kizayuni wa Israel usijilimbikizie silaha hizo hatari na angamizi.