Al Houthi: Marekani inakasirishwa na mapambano dhidi ya magaidi wa Daesh
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i71914-al_houthi_marekani_inakasirishwa_na_mapambano_dhidi_ya_magaidi_wa_daesh
Mkuu wa Baraza Kuu la Kisiasa la Yemen amesema kuwa, Marekani inafanya mazungumzo na wakati huo huo inayaunga mkono na kuyahami makundi ya kigaidi ya al Qaida na Dash na kukasirishwa na mapambano ya taifa la Yemen dhidi ya makundi hayo.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jul 02, 2021 06:36 UTC
  • Muhammad Ali al Houthi
    Muhammad Ali al Houthi

Mkuu wa Baraza Kuu la Kisiasa la Yemen amesema kuwa, Marekani inafanya mazungumzo na wakati huo huo inayaunga mkono na kuyahami makundi ya kigaidi ya al Qaida na Dash na kukasirishwa na mapambano ya taifa la Yemen dhidi ya makundi hayo.

Hayo yamesemwa leo Ijumaa na Muhammad Ali al Houthi ambaye pia amekosoa hatua ya Marekani, Uingereza, Saudi Arabia, Imarati na washirika wao dhidi ya watu wa Yemen. 

Al Houthi amesema kuwa, taifa la Yemen limechoshwa na matamshi na maneno matupu kuhusu amani yanayotolewa kila siku na nchi zinazoendelea kushambulia raia wa nchi hiyo kwa mabomu na kulizingira taifa la Yemen.

Muhammad Ali al Houthi amesema kuwa, silaha za Marekani zinazouzwa kwa Saudia na washirika wake ndiyo sababu kuu ya kuendelea vita na kukaliwa kwa mabavu ardhi ya Yemen na kuongeza kuwa, mashaka ya watu wa Yemen yatakoma baada ya Marekani kusitisha mashambulizi na kukomesha kukalia kwa mabavu baadhi ya ardhi ya nchi hiyo na kuwazingira Wayemeni. 

Kwa sasa mji wa Marib huko kaskazini mwa Yemen unahesabiwa kuwa ngome ya mwisho ya mamluki na vibaraka wa Saudi Arabia, Imarati na washirika wao. Katika miezi ya karibuni jeshi la Yemen na wapiganaji wa kujitolea wa harakati ya Ansarullah wamewafanikiiwa kukomboa sehemu kubwa ya mkoa huo na kuwafukuza au kuwaangamiza mamluki wa Saudia katika eneo hilo.