Ansarullah: Wavamizi wamepata kipigo kikali katika mkoa wa al Bayda' Yemen
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i72170-ansarullah_wavamizi_wamepata_kipigo_kikali_katika_mkoa_wa_al_bayda'_yemen
Msemaji wa Harakati ya Kujitolea ya Wananchi wa Yemen maarufu kwa jina la Ansarullah amesema kuwa, askari wa muungano vamizi unaoongozwa na Saudi Arabia wamepata kipigo kikali katika mkoa wa al Bayda' kutoka kwa jeshi la Yemen na vikosi vya kujitolea vya wananchi wa nchi hiyo.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jul 09, 2021 08:17 UTC
  • Wanamapambano wa Ansarullah katika vita vya ukombozi nchini Yemen.
    Wanamapambano wa Ansarullah katika vita vya ukombozi nchini Yemen.

Msemaji wa Harakati ya Kujitolea ya Wananchi wa Yemen maarufu kwa jina la Ansarullah amesema kuwa, askari wa muungano vamizi unaoongozwa na Saudi Arabia wamepata kipigo kikali katika mkoa wa al Bayda' kutoka kwa jeshi la Yemen na vikosi vya kujitolea vya wananchi wa nchi hiyo.

Hayo yameripotiwa leo Ijumaa na shirika la habari la ISNA na kumnukuu Mohammad Abdul Salaam akisema kwenye mtandao wa kijamii wa Twitter kwamba, muungano vamizi unaoongozwa na Saudia haujapata chochote ghairi ya kipigo katika medani zote na kwenye viwango vyote.

Siku chache zilizopita pia, Kaimu Mkuu wa Majeshi ya Yemen alisema kuwa, wanajeshi wa Marekani ndio wanaoongoza vita katika mkoa wa al Bayda' wakishirikiana na magaidi wa al Qaida, Daesh (ISIS) na Jabhat al Nusra.

Wavamizi wanaoongozwa na Saudia wanafanya jinai kubwa dhidi ya wananchi wa Yemen. Hapa ni katika shambulio la kinyama dhidi ya Waislamu waliokuwa wanasali msikitini huko Yemen

 

Shirika la habari la SABA la Yemen lilitangaza habari hiyo na kumnukuu Meja Jenerali Ali Hamud al Mushki, akifichua uhakika huo na kuongeza kuwa, wakati wanajeshi wa Marekani walipochukua jukumu la kuongoza vita dhidi ya wanajeshi wa Yemen katika mkoa wa al Bayda', wananchi na jeshi la Yemen limevunja jeuri na majigambo ya Marekani na utawala wa Kizayuni wa Israel wanaoongoza vibaraka na maluki wao kufanya jinai dhidi ya wananchi wa Yemen.

Meja Jenerali al Mushki vile vile alisema kuwa, wavamizi watatimuliwa wote katika kila shibri ya ardhi ya Yemen na kipigo watakachopata ni kichungu sana kuliko walichopata wavamizi waliowatangulia hawa wa hivi sasa.

Jumapili wiki hii, makamanda kadhaa wa genge la al Qaida waliangamizwa katika mashambulizi ya mizinga ya Harakati ya Kujitolea ya Wananchi wa Yemen maarufu kwa jina la Ansrullah, kwenye mkoa wa al Bayda' ulioko umbali wa kilomita 209 mashariki mwa mji mkuu, San'a.