Wanajeshi wa Marekani waendelea kupora mafuta ya Syria
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i73346-wanajeshi_wa_marekani_waendelea_kupora_mafuta_ya_syria
Wanajeshi vamizi wa Marekani wanaendelea kupora mafuta ghafi ya petroli katika maeneo wanayoyakalia kwa mabavu nchini Syria.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Aug 10, 2021 03:03 UTC
  • Wanajeshi wa Marekani waendelea kupora mafuta ya  Syria

Wanajeshi vamizi wa Marekani wanaendelea kupora mafuta ghafi ya petroli katika maeneo wanayoyakalia kwa mabavu nchini Syria.

Shirika Rasmi la Habari la Syria (SANA) limeripoti Jumatatu kuwa askari wa jeshi la kigaidi la Marekani wamepora trela 80 za mafuta ya Syria kupitia kivuko cha mpakani kinachotumiwa kinyume cha sheria cha Al Waleed na kuelekea kaskazini mwa Iraq. 

Hivi karibuni Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Russia Maria Zakharova alisema Marekani inachukua kinyume cha sheria mafuta ghafi ya petroli yenye thamani ya dola milioni 30 kwa mwezi kutoka visima vya mafuta vilivyoko kaskazini mashariki mwa Syria.

Jeshi la Marekani ambalo linashirikiana na makundi ya kigaidi kwa muda mrefu limeweka kambi kinyume cha sheria katika maeneo ya kaskazini na mashariki mwa Syria. Mbali na kupora mafuta ghafi ya petroli na ngano, limekuwa pia likishambulia askari na watu wa Syria. Marekani ni muuungaji mkono mkuu wa makundi ya kigaidi nchini Syria. 

Magaidi wanaopata himaya ya Marekani

Mgogoro wa Syria ulianza mwaka 2011 wakati magaidi waliokuwa wakipata himaya ya Saudia, Marekani na waitifaki wao walipoanzisha vita dhidi ya serikali ya Rais Bashar al Assad. Lengo la vita hivyo lilikuwa ni kuiangusha serikali halali ya Syria ili kubadilisha mlingano wa nguvu katika eneo kwa maslahi ya utawala wa Kizayuni. Hata hivyo njama hiyo imefeli kwani serikali ya Syria kwa msaada wa waitifaki wake imefanikiwa kuwatimua magaidi hao katika aghalabu ya maeneo ya nchi hiyo.