Ripoti: Iraq inapanga mkutano wa Iran na Saudi Arabia mjini Baghdad
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i73348-ripoti_iraq_inapanga_mkutano_wa_iran_na_saudi_arabia_mjini_baghdad
Duru za habari zinadokeza kuwa maafisa wa serikali ya Iraq wanaandaa mkutano baina ya maafisa wa Iran na Saudi Arabia pembizoni nwa Kongamano la Baghdad la Usalama wa Kieneo.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Aug 10, 2021 03:06 UTC
  • Ripoti: Iraq inapanga mkutano wa Iran na Saudi Arabia mjini Baghdad

Duru za habari zinadokeza kuwa maafisa wa serikali ya Iraq wanaandaa mkutano baina ya maafisa wa Iran na Saudi Arabia pembizoni nwa Kongamano la Baghdad la Usalama wa Kieneo.

Kwa mujibu wa Televisheni ya Al Mayedeen, kati ya nchi zitakazoshiriki katika kongamano hilo la Baghdad baadaye mwezi huu ni pamoja na Iran, Saudi Arabia, Uturuki, Umoja wa Falme za Kiarabu, Qatar, Misri and Jordan, na Iraq. Aidha Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa pia anatazamiwa kushiriki katika kongamano hilo.

Televisheni ya Al Mayedeen imesema kunafanyika jitihada za kuzikutanisha Iran na Saudi Arabia pembizoni mwa kikao hicho. Taarifa hiyo imesema Iraq imekuwa mstari wa mbele katika kuzipatanisha Iran na Saudi Arabia baada ya uhusiano wa nchi mbili kuvunjika miaka kadhaa iliyopita.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iraq Fuad Mohammed Hussein

Hayo yanaripotiwa wakati ambao Waziri wa Mambo ya Nje wa Iraq Fuad Mohammed Hussein leo anatazamiwa kuwasili Tehran na kufanya mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Mohammad Javad Zarif pamoja na maafisa wengine wa ngazi za juu nchini Iran.

Jana waziri huyo wa mambo ya nje wa Iraq alikuwa mjini Riyadh Saudi Arabia ambapo alikutana na kufanya mazungumzo na wawziri wa mambo ya nje wa ufalme huo Faisal Bin Farhan.