Jeshi la Yemen latungua droni ya ujasusi ya Marekani
-
Scan Eagle
Msemaji wa Jeshi la Yemen amesema kuwa jeshi hilo limetungua droni ya ujasusi ya Marekani katika mkoa wa Ma'rib.
Brigedia Jenerali Yahya Saree amesema kuwa vikosi vya ulinzi vya nchi hiyo leo Jumatatu vimetungua ndege isiyo na rubani (droni) ya ujasusi ya Marekani aina ya Scan Eagle kwa kutumia kombora la ardhi kwa anga. Saree ameongeza kuwa, droni hiyo imetunguliwa ikiwa katika oparesheni za kiadui katika anga ya Madghal katika mkoa wa Ma'rib.
Brigedia Jenerali Yahya Saree amesema kuwa, kituo cha habari la Al I'lam al Harbi kimerekodi oparesheni hiyo ya kutunguliwa droni ya ujasusi ya Marekani na kwamba hivi karibuni kitaonyesha picha ya vipande vya droni hiyo. Hii si mara ya kwanza kwa jeshi la Yemen kuripoti habari ya ujasusi wa ndege zisizo na rubani za Marekani katika anga ya nchi hiyo.
Jeshi hilo mwezi uliopita pia lilitungua ndege nyingine ya ujasusi ya Marekani aina ya Scan Eagle mkoani Ma'rib.
Droni hiyo aina ya Scan Eagle ni ndege isiyo na rubani iliyotengenezwa na kampuni ya Incito ina thamani ya dola milioni 11. 25.