Hamas: Kukiri kushindwa Israel kunadhihirisha nguvu ya muqawama
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i73556-hamas_kukiri_kushindwa_israel_kunadhihirisha_nguvu_ya_muqawama
Msemaji wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) amesema hatua ya utawala wa Kizayuni wa Israel ya kukiri kushindwa katika vita vya karibuni huko Ghaza inadhihirisha nguvu iliyonayo wanamapambano wa Palestina.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Aug 15, 2021 22:06 UTC
  • Hamas: Kukiri kushindwa Israel kunadhihirisha nguvu ya muqawama

Msemaji wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) amesema hatua ya utawala wa Kizayuni wa Israel ya kukiri kushindwa katika vita vya karibuni huko Ghaza inadhihirisha nguvu iliyonayo wanamapambano wa Palestina.

Abdullatif al Qanuu amesisitiza kuwa, kukiri utawala ghasibu za Israel, makamanda wa kijeshi na taasisi za utawala huo kuwa walishindwa kukabiliana na muqawama wa Palestina na kufeli katika vita vya Seif al Quds kunaonyesha nguvu na uwezo wa muqawama na uwezekano wa kusonga mbele zaidi wanamapambano wa Palestina katika vita na utawala ghasibu wa Israel. Amesema, kukiri huko kunadhihirisha namna muqawama ulivyofichua malengo ya kihabithi ya Israel. 

Al Qanu ameongeza kuwa, suala hilo limethibitisha pia uwezo wa muqawama wa kujibu mashambulizi ya adui. 

Hazim Qassim ambaye pia ni Msemaji wa Hamas amesisitiza kuwa, wanaendelea kuwasiliana na wapatanishi ili kuishawishi Israel iondoe kikamilifu mzingiro dhidi ya Ghaza. 

Qassim amesema Hamas inaendelea kuwasiliana na wapatanishi tangu mwezi Mei mwaka huu hususan ndugu zao wa Misri ili kuondoa mzingiro wa Ghaza na vizuizi vyote vilivyowekwa na Israel. 

Ukanda wa Ghaza uko chini ya mzingiro wa anga, nchi kavu na bahari uliowekwa na Israel tangu mwaka 2006. Mzingiro huo umesababisha matatizo na masaibu chungu nzima kwa wakazi wa Kipalestina wa eneo hilo.