OIC yalaani jinai iliyofanywa na wanajeshi wa Israel huko Jenin
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i73628-oic_yalaani_jinai_iliyofanywa_na_wanajeshi_wa_israel_huko_jenin
Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC) imelaani jinai iliyofanywa na wanajeshi wa utawala wa Kizayuni wa Israel ya kuwaua shahidi vijana wanne wa Kipalestina katika eneo la Jenen.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Aug 17, 2021 22:10 UTC
  • OIC yalaani jinai iliyofanywa na wanajeshi wa Israel huko Jenin

Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC) imelaani jinai iliyofanywa na wanajeshi wa utawala wa Kizayuni wa Israel ya kuwaua shahidi vijana wanne wa Kipalestina katika eneo la Jenen.

Taarifa iliyotolewa na OIC imesema kuwa, jinai ya kutisha ya wanajeshi wa Israel ya kuwaua shahidi vijana wanne wa Kipalestina katika mji wa Jenin imekiuka sheria za kimataifa, haki za binadamu na mikataba ya kimataifa.

Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu imesisitiza katika taarifa hiyo kwamba utawala wa Kizayuni wa Israel kama dola vamizi, unabeba dhima ya machafuko hatari yanayoshuhudiwa katika eneo hilo.

OIC pia imeitaka jumuiya ya kimataifa kutekeleza majukumu yake ya kuwahami raia wa Palestina, kuilazimisha Israel isitishe mashambulizi yake dhidi ya raia na kuheshimu majukumu yake ya kimataifa. 

Wizara ya Afya ya Palestina ilitangaza jana kwamba, vijana wanne wa Kipalestina wameuawa shahidi katika hujuma ya wanajeshi wa Israel kwenye eneo la Jenin lililoko Ukingo wa Magharibi mwa Mto Jordan. Taarifa ya wizara hiyo imesema wanajeshi wa Israel wamechukua maiti za vijana wawili kati ya nne za Wapalestina hao.