Palestina yakosoa kimya cha walimwengu kwa jinai za Wazayuni
Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Mamlaka ya Ndani ya Palestina imekosoa vikali kimya cha jamii ya kimataifa kwa jinai za kila leo za utawala haramu wa Israel.
Taarifa ya Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Mamlaka ya Ndani ya Palestina imeashiria kitendo cha utawala ghasibu wa Israel cha kuchukua mateka miili ya mashahidi wa Kipalestina na kueleza kwamba, kimya cha jamii ya kimataifa mbele ya jinai hizi ni ishara ya wazi kwamba, linapojitokeza suala la Israel kutenda jinai, jamii ya kimataifa huwa haitekelezi majukumu yake kama inavyotakiwa.
Sehemu nyingine ya taarifa ya Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Mamlaka ya Ndani ya Palestina imeeleza kwamba, Wapalestina walitaraji kwamba, baada ya kitendo hiki cha kinyama cha Israel jamii ya kimataifa na mashirika ya kutetea haki za binadamu yatajitokeza kutetea haki na uadilifu.
Hatua ya utawala haramu wa Israe ya kutokabidhi miili ya Wapalestina waliouawa shahidi kwa ajili ya mazishi bila shaka ni mwendelezo wa sera zake za tangu na tangu, na kitendo hicho ni utendaji wa wazi wa jinai dhidi ya binadamu, imeeleza sehemu nyingi ya taarifa hiyo ya Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Mamlaka ya Ndani ya Palestina.
Wapalestina wanne waliuawa shahidi kwa kupigwa risasi na Israel Jumatatu iliyopita na hadi sasa utawala huo umekataa kukabidhi miili ya mashahidi wawili kwa Kipalestina kwa ajili ya mazishi.