Ripoti: Muungano vamizi wa Saudi Arabia wakiuka usitishaji vita mara 339
Chumba cha Operesheni cha Maafisa wa Jeshi la Yemen kimetangaza kuwa, muungano vamizi unaoongozwa na utawala vamizi wa Saudi Arabia pamoja na mamluki wao umekiuka usitishaji vita nchini Yemen mara 339.
Taarifa hiyo imeeleza kuwa, majeshi vamizi ya muungano unaoongozwa na utawala vamizi wa Saudi Arabia yamekiuka usitishaji vita mara 339 katika kipindi cha masaa 24 yaliyopita huko katika mji wa bandari wa Al-Hudaydah ulioko magharibi mwa mwa Yemen.
Kwa mujibu wataarifa ya Chumba cha Operesheni cha Maafisa wa Jeshi la Yemen ni kuwa, katika ukiukaji huo wa usitishaji vita, majeshi vamizi yameushambulia mji huo kwa silaha nyepesi na nzito.
Usitishaji vita katika mkoa wa al-Hudaydha ulianza kutekelezwa Disemba 18 mwaka 2018 katika mkoa wa al-Hudaydah, hata hivyo muungano vamizi unaoongozwa na Saudi Arabia umekuwa ukikiuka kila siku usitishaji vita huo.
Saudi Arabia huku ikungwa mkono na Marekani na nchi nyingine kadhaa, Machi 25 mwaka 2015 zilianzisha hujuma na mashambulizi makubwa huko Yemen na kuiwekea nchi hiyo mzingiro wa baharini, angani na nchi kavu.
Vita hivyo vya kidhulma vya Saudia na waitifaki wake huko Yemen hadi sasa vimesababisha kuuliwa maelfu ya Wayemeni, kujeruhiwa makumi ya maelfu na kuwa wakimbizi mamilioni ya wengine.
Aidha asasi na jumuiya mbalimbali za misaada ya kibinadamu zimetahadharisha mara chungu nzima kuhusiana na hali mbaya ya kibinadamu inayoikabili Yemen na hata uwezekano wa kutokea maafa ya kibinadamu katika nchi hiyo.