Makumi ya askari wa muungano wa Saudia wauawa Ma'rib, Yemen
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i74152-makumi_ya_askari_wa_muungano_wa_saudia_wauawa_ma'rib_yemen
Makumi ya askari na mamluki wa vikosi vya waitifaki wa Saudi Arabia wameangamizwa katika makabiliano na jeshi la Yemen likishirikiana na vikosi vya kujitolea wananchi.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Sep 01, 2021 02:45 UTC
  • Makumi ya askari wa muungano wa Saudia wauawa Ma'rib, Yemen

Makumi ya askari na mamluki wa vikosi vya waitifaki wa Saudi Arabia wameangamizwa katika makabiliano na jeshi la Yemen likishirikiana na vikosi vya kujitolea wananchi.

Duru za kijeshi zimeripoti kuwa, idadi kubwa ya askari waitifaki wa serikali iliyojiuzulu ya Yemen na wanaopatiwa himaya na Saudia wameuawa ndani ya saa chache zilizopita katika mkoa wa kistratijia wa Ma'rib.

Habari zaidi zinasema kuwa, makamanda wa muungano huo vamizi ni miongoni mwa askari waliouawa, huku wengine wengi wakijeruhiwa.

Haya yanajiri katika hali ambayo, ripoti zinasema jeshi la Yemen linakaribia kuudhibiti tena mji Ma’rib ambao ni makao makuu ya mkoa huo wa kistratijia. Jeshi na harakati ya kujitolea ya wananchi wa Yemen jana Jumanne walisonga mbele kwa kiasi kikubwa na kukaribia mahali zilipo idara za serikali za mji wa  Ma’rib.  

Mwanamapambano wa Ansarullah akivurumisha kombora

Magaidi hao wanaopewa himaya na Saudia, wamelazimika kuziacha ngome zao kufuatia mashambulizi makali ya jeshi na harakati ya kujitolea ya wananchi wa Yemen. 

Siku chache zilizopita, askari wasiopungua 30 wa muungano wa kijeshi unaoongozwa na Saudi Arabia waliangamizwa na wengine 60 kujeruhiwa katika shambulio lililofanywa na wapiganaji wa harakati ya Ansarullah dhidi ya kituo kikubwa zaidi cha kijeshi cha muungano huo vamizi kusini mwa Yemen.