Wapinzani wa kuanzishwa uhusiano wa kawaida na Israel wanatiwa mbaroni Saudia
Asasi moja ya kutetea haki za binadamu nchini Saudi Arabia imetangaza kuwa, vyombo vya usalama vya nchi hiyo vinawatia mbaroni wale wote wanaopinga kuanzishwa uhusiano wa kawaida na utawala haramu wa Kizayuni wa israel.
Asasi ya ALQST for Human Rights inayojihusisha na masuala ya haki za binadamu nchini Saudia imetangaza kuwa, Abdallah al-Yahya anashikiliwa kizuizini tangu tarehe 24 ya mwezi uliopita wa Disemba kwa kosa la kuandika katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Twitter ujumbe wa kukosoa mwenendo wa mataifa ya Kiarabu wa kuanzisha uhusiano wa kawaida na utawala bandia wa Israel.
Ripoti kutoka Saudia zinasema kuwa, Abdallah al-Yahya siyo raia wa kwanza wa nchi hiyo kutiwa mbaroni na kushikiliwa kizuizini kwa kosa la kuunga mkono taifa la Palestina na kupinga kuanzishwa uhusiano wa kawaida na utawala dhalimu wa Israel.
Kabla ya hapo, vikosi vya usalama vya Saudia vimewatia mbaroni makumi ya wasomi wa vyuo vikuu, wanazuoni na wanaharakati wa mtandao wa kijamii wa twitter kwa kosa la kutangaza kupinga kuanzishwa uhusiano wa kawaida na utawala ghasibu wa Israe.
Aprilii mwaka jana (2021) Mahakama ya Jinai ya Saudi Arabia ilimhukkumu kifungo cha miaka mitano jela Abdul-Aziz al-Awdah mwanaharakari mashuhuri katika mtandao wa kijamii wa twiitter kwa kosa la kutetea malengo ya Palestina na kupinga hatua ya baadhi ya mataifa ya Kiarabu ya kuwasaliti Wapalestina na kuanzisha uhusiano wa kawaida na utawala vamizi wa Israel unaofanya mauaji na ukatili kila leo dhidi ya wananchi madhulumu wa Palestina.