Jeshi la Saudia laua wanawake na watoto wanne wa Yemen
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i78990-jeshi_la_saudia_laua_wanawake_na_watoto_wanne_wa_yemen
Jeshi la utawala vamizi wa Saudia limevurumisha mabomu katika nyumba za raia nchini Yemen na kuua wanawake na watoto wanne.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jan 09, 2022 04:30 UTC
  • Jeshi la Saudia laua wanawake na watoto wanne wa Yemen

Jeshi la utawala vamizi wa Saudia limevurumisha mabomu katika nyumba za raia nchini Yemen na kuua wanawake na watoto wanne.

Televisheni ya Al Masirah imeripoti kuwa mizinga ya Saudia ilivurumisha mabomu katika mji wa Muqbanah mkoani Ta'iz kusini mwa Yemen Jumamosi jioni na kusbabaisha hasara kubwa.

Kwa mujibu wa taarifa wanawake wawili na watoto wawili wameuawa katika hujuma hiyo ya kinyama huku wasichana wengine wawili wachanga wakijeruhiwa vibaya.

Katika tukio jingine Jumamosi asubuhi, ndege za kivita za Saudia zilishamulia eneo la Sa'ada kaskazini mwa Yemen na kuua raia wawili na kuwajeruhi wengine kadhaa.

Kufuatia uungaji mkono wa Marekani, Imarati, utawala haramu wa Israel na nchi nyingine kadhaa za Kiarabu, Saudi Arabia iliivamia kijeshi nchi masikini ya Yemen mnamo Machi 2015 na kuiwekea mzingiro wa pande zote wa nchi kavu, anga na majini. Uvamizi wa kijeshi wa Saudia umeisababishia pia Yemen uhaba mkubwa wa chakula na dawa. 

Watoto ni waathirika wakuu wa vita vinavyoongozwa na Saudia dhidi ya Yemen

Hivi karibuni  Shirika la Entesaf la Kupigania Haki za Wanawake na Watoto lenye makao yake nchini Yemen, limesema watoto zaidi ya 300 wa Kiyemen wanaaga dunia kila siku kutokana na utapiamlo wa kiwango cha juu, hali ambayo imesababishwa na vita vya Saudia dhidi ya nchi hiyo.

Hadi hivi sasa uvamizi huo wa Saudia na waitifaki wake umeshasababisha malaki ya Wayemen kuuawa, wengine wengi kujeruhiwa huku mamilioni ya wengine wakiwa wakimbizi ndani na nje ya nchi.