Marekani yajenga kiwanda cha kusafishia mafuta ya kuiba huko Hasakah, Syria
Wanajeshi magaidi wa Marekani pamoja na wanamgambo wenye mfungamano nao wamejenga kiwanda cha kusafishia mafuta huko Hasakah nchini Syria kwa lengo la kuiba mafuta ya nchi hiyo.
Wanajeshi vamizi wa Marekani wanaoshirikiana na makundi ya waasi wa Kikurdi wa SDF wamejenga kiwanda cha kusafishia mafuta karibu na kisima cha mafuta cha Ramilan katika mkoa wa Hasakah chenye uwezo wa kusafisha mapipa elfu tatu ya mafuta kwa siku.
Baada ya ujenzi wa kiwanda hicho, inatarajiwa kuwa katika wiki na miezi ijayo kutashuhudiwa ongezeko kubwa la vitendo vya wizi na uporaji wa mafuta ya Syria kutoka eneo la mashariki mwa nchi hiyo kunakofanywa na wanajeshi vamizi wa Marekani.
Katika upande mwingine, wanajeshi vamizi wa Marekani juzi Jumamosi wakiongozana na msafara wa malori 79 yalikuwa yamebeba mafuta yaliyoibwa Syria na malori mengine kadhaa walionekana wakielekea upande wa kaskazini mwa Iraq. Wanajeshi vamizi wa Marekani wanaiba mafuta ya Syria na kuyatumia huku serikali na wananchi wa Syria wenyewe wakikabiliwa na uhaba wa mafuta. Baadhi ya wakati malori yameonekana yakisubiri kwa masaa kadhaa kujaza mafuta.
Serikali ya Syria inakutaja kuwepo wanajeshi wa Marekani kaskazini mashariki na kusini mashariki mwa nchi hiyo kuwa ni uvamizi.