HAMAS: Vitisho vya Wazayuni vinatokana na kuchanganyikiwa kwao
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i83360-hamas_vitisho_vya_wazayuni_vinatokana_na_kuchanganyikiwa_kwao
Msemaji wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS amesema kuwa, njama za Wazayuni za kutaka kuwaua viongoz wa harakati hiyo huko Gaza ni ishara ya wazi ya kuchanganyikiwa utawala ghasibu wa Israel baada ya operesheni ya kimuqawama ya Tel-Aviv.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
May 07, 2022 06:44 UTC
  • HAMAS: Vitisho vya Wazayuni vinatokana na kuchanganyikiwa kwao

Msemaji wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS amesema kuwa, njama za Wazayuni za kutaka kuwaua viongoz wa harakati hiyo huko Gaza ni ishara ya wazi ya kuchanganyikiwa utawala ghasibu wa Israel baada ya operesheni ya kimuqawama ya Tel-Aviv.

Hazim Qassim, msemaji wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS sambamba na kuwabebesha Wazayuni dhima ya yale yaliyotokea Tel Aviv ikiwa ni natija ya hujuma na mashambulio dhidi ya msikiti wa al-Aqswa amesisitiza kuwa, njia ya muqawama na mapambano dhidi ya wavamizi katu haitasimama.

Hivi karibuni Wapalestina walitekeleza operesheni nyingine katika kitongoji cha walowezi cha El'ad huko Mashariki mwa Tel Aviv ambapo wazayuni watatu waliangamizwa na wengine wanne wamejeruhiwa.

Maafisa wa Kizayuni wa Israel wamembebesha lawama za operesheni hiyo Yahya Sinwar ambaye ni miongoni mwa maafisa wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) na wametoa wito wa kuuawa kwake.

Katika hotuba yake kwenye maandamano ya Siku ya Kimataifa ya Quds kwenye Ijumaa ya mwisho ya mwezi wa Ramadhani, Sinwar alipongeza operesheni za Wapalestina katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu na Wazayuni.

Wazayuni 3 waaangamizwa katika Oparesheni ya Siku ya Nakba huko Elad 

 

Waziri wa Usalama wa Ndani wa utawala wa Kizayuni amenukuliwa akikiri hasara kubwa iliyopata Israel kutokana na operesheni ya kishujaa ya wanamapambano wa Palestina katika kitongoji cha El'ad cha mashariki mwa Tel Aviv na kusema kuwa, tumepata hasara kubwa katika operesheni hiyo.

Wanamapambano wa Palestina wametangaza wazi kwamba, hawatishwi na vitisho vya Israel vya kuwaua viongozi wao na kwamba, muqawama dhidi ya Wzayuni utaendelea.