Jihad al Islami yawapongeza Wapalestina kwa muqawama wao imara
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i83612-jihad_al_islami_yawapongeza_wapalestina_kwa_muqawama_wao_imara
Katibu Mkuu wa Harakati ya Jihad al Islami ya Palestina amewapongeza Wapalestina kwa muqawama imara na kusimama kidete kukabiliana na jinai za Wazayuni.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
May 14, 2022 06:26 UTC
  • Jihad al Islami yawapongeza Wapalestina kwa muqawama wao imara

Katibu Mkuu wa Harakati ya Jihad al Islami ya Palestina amewapongeza Wapalestina kwa muqawama imara na kusimama kidete kukabiliana na jinai za Wazayuni.

Kituo cha Upashaji Habari cha Palestina kimemnukuu Ziyad al Nakhalah akisema hayo katika mazungumzo ya simu na baba wa mateka wa Kipalestina waliotekwa nyara jana na kupelekwa katika jela za kuogofya za utawala wa Kizayuni wa Israel na kusema kuwa, Harakati ya Jihad al Islami inajivunia wanamapambano hao wa Kipalestina.

Ijumaa ya jana, wanajeshi makatili wa utawala wa Kizayuni wa Israel walivamia nyuma na mateka hao wa Kipalestina Mahmoud al Dabai na  nduguye na kuwapeleka kusikojulikana.

Wakati wa uvamizi huo, Wapalestina walipambana kiume na wanajeshi makatili wa Israel na kumwangamiza mwanajeshi mmoja Mzayuni na kujeruhi wengine watatu.

Brigedi za al Quds huko Jenin

 

Mwanamapambano huyo na ndugu yake aliyejulikana Anas al Dabai alitekwa nyara na Wazayuni baada ya kutokea mapigano makali huko Jenin, Katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan.

Taarifa zinasema kuwa, Wapalestina wasiopungua 13 wamejeruhiwa kwenye uvamizi huo wa Wazayuni baada ya wanamapambano wa Palestina kupambana kiume na wanajeshi makatilii wa Israel.

Katibu Mkuu wa Harakati ya Jihad al Islami ya Palestina amempongeza baba wa mateka hao wawili, Muhammad al Dabai kwa kutoka salama katika uvamizi huo na kusisitiza kuwa mapambano ya Wapalestina hao ni fakhari kwa taifa zima la Palestina.

Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palesitna HAMAS pamoja na Harakati ya Taifa ya Ukombozi wa Palestina nazo zimetoa matamko tofauti na kuwapongeza wananchi wa Jenin kwa kupambana kiume na wanajeshi dhalimu wa Israel.