Ripoti: Wanaharakati wa kisiasa Saudia wanabakwa na kuuawa magerezani
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i85192-ripoti_wanaharakati_wa_kisiasa_saudia_wanabakwa_na_kuuawa_magerezani
Ripoti mpya iliyotolewa na shirika la kutetea haki za binadamu la Grant Liberty kwa mara nyingine tena imeweka wazi rekodi mbaya na nyeusi ya utawala wa Saudi Arabia katika suala la haki za binadamu, hususan baada ya Muhammad Bin Salman, Mrithi wa Ufalme Saudia kuchukua udhibiti wa mamlaka.
(last modified 2026-03-17T04:36:21+00:00 )
Jun 26, 2022 06:46 UTC
  • Ripoti: Wanaharakati wa kisiasa Saudia wanabakwa na kuuawa magerezani

Ripoti mpya iliyotolewa na shirika la kutetea haki za binadamu la Grant Liberty kwa mara nyingine tena imeweka wazi rekodi mbaya na nyeusi ya utawala wa Saudi Arabia katika suala la haki za binadamu, hususan baada ya Muhammad Bin Salman, Mrithi wa Ufalme Saudia kuchukua udhibiti wa mamlaka.

Ripoti ya shirika hilo lenye makao yake nchini Uingereza imefichua kuwa, miongoni mwa wafungwa 311 wa itikadi katika jela na magereza ya Saudia, 53 wamekabiliwa na mateso ya kutisha, sita wamebakwa na kudhalilishwa kingono, na 14 walilazimishwa kuingia katika mgomo wa kula.

Uchunguzi wa shirika la kutetea haki za binadamu la Grant Liberty la Uingereza umefichua kuwa, wafungwa 22 walikamatwa kwa jinai ambazo walizifanya wakiwa watoto wadogo.

Ripoti hiyo imeongeza kuwa, wafungwa kumi na watatu wa itikadi wanakabiliwa na hukumu ya kunyongwa, na wengine wanne tayari wamekwishanyongwa.

Imesema hata watu ambao walikuwa wafungwa na kuachiwa huru sasa wamewekewa vizuizi na hawaruhusiwi kufanya safari nje ya nchini Saudia

Shirika hilo limesema Saudi Arabia imezidisha ukandamizaji na kuwatesa wanaharakati wa kupigania haki za binadamu na haki za kiraia na kwamba idadi ya watu walionyongwa nchini humo pia imeongezeka sana katika kipindi cha miezi michache iliyopita.