Wabahrain waandamana kulalamikia kuanzisha uhusiano wa kawaida na Israel
Wananchi wa Bahrain wameandamana kulalalamikia na kulaani hatua ya nchi yao ya kuanzisha uhusiano wa kawaida na utawala haramu wa Israel.
Maandamano hayo makubwa yaliyofanyika katika mji mkuu Manama yalishuhudia waandamanaji wakiwa wamebeba mabango na maberamu huku wakipiga nara za kuulaani utawala ghasibu wa Israel unaofanywa mauaji kila leo huko Palestina inayokaliwa kkwa mabavu.
Waandamanaji hao wameutakka utawala wa Manama kuvunja makubaliano yake na Israel ya kuanzisha uhusiano wa kawaida ambayo wanasema ni khiyana na usaliti kwa taifa madhulumu la Palestina na ulimwengu wa Kiislamu kwa ujumla.
Bahrain ilitia saini makubaliano ya kuanzisha uhusiano wa kawaida na utawala haramu wa Israel chini ya usimamizi wa Marekani katika Ikulu ya White House mnamo Septemba 2020.
Tangu wakati huo, tawala za Manama na Tel Aviv zimekuwa zikijaribu kuimarisha uhusiano huku Wapalestina na wafuasi wao wa kieneo na kimataifa wakiutaja uhusiano huo kuwa ni usaliti kwa harakati ya kupigania ukombozi wa ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu na Israel.
Mwezi Disemba mwaka 2020 Morocco ilijiunga na Imarati, Bahrain na Sudan katika kuanzisha uhusiano rasmi na utawala haramu wa Israel chini ya upatanishi wa Marekani.
Mapatano hayo yanaendelea kulaaniwa ndani ya nchi hizo za Kiarabu na ulimwengu wa Kiislamu kwa ujumla kwani fikra za waliowengi zinaamini kuwa ni usaliti kwa malengo matukufu ya ukombozi wa Palestina.