-
HAMAS yatumia droni iliyoiteka kutoka kwa Israel kuwatwanga Wazayuni
Dec 30, 2024 23:24Brigedi za Izzudin Qassam, Tawi la Kijeshi la Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS zimetangaza kuwa, zimetumia droni ziliyoiteka kutoka kwa wanajeshi wa Israel kuwashambulia wanajeshi hao vamizi na Wazayuni wenzao.
-
Wanajeshi wa Israel waendelea kupokea vipigo kutoka kwa wanamapambano wa Palestina
Dec 30, 2024 23:21Kundi la Saraya al-Quds, Tawi la Kijeshi la Harakati ya Jihad al Islami ya Palestina, limetangaza kwamba limefanikiwa kutoa kipigo kipya na kikali mno kwa wanajeshi makatili na vamizi wa Israel huko Ghaza.
-
UN yataka kusaidiwa mfumo wa afya wa Ukanda wa Gaza
Dec 30, 2024 08:52Msemaji wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amebainisha wasiwasi wake kuhusu hujuma ya Israel katika hospitali ya Kamal Adwan kaskazini mwa Ukanda wa Gaza na kutaka kusaidia mfumo wa matibabu katika eneo hilo.
-
Wanajeshi 40 wa Israel waangamizwa kaskazini mwa Gaza
Dec 30, 2024 04:25Makundi ya muqawama ya Wapalestina yanaendelea na operesheni zao dhidi ya jeshi katili la Israel kwa kuvurumisha makombora zaidi kwenye ngome za utawala wa Israel katika maeneo yanayokaliwa kwa mabavu.
-
Jeshi la Yemen limetekeleza operesheni 13 za makombora dhidi ya Israel ndani ya siku 10
Dec 30, 2024 04:22Msemaji wa Jeshi la Yemen amesema kwamba vitengo vya makombora vya nchi hiyo vimeendesha angalau operesheni 13 dhidi ya ngome za utawala wa Kizayuni wa Israel katika siku 10 zilizopita. Operesheni hizo zinatekelezwa kulipiza kisasi kwa niaba ya Wapalestina katika Gaza ambao wanakabiliwa na mauaji ya kimbari vya utawala wa Kizayuni wa Israel.
-
Hamas yaonya kuhusu sera za Israel za kujitanua
Dec 30, 2024 04:21Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina, Hamas, imeonya kuhusu sera ya kujitanua ya utawala haramu wa Israel nchini Syria kufuatia kuanguka kwa Rais wa zamani wa nchi hiyo, Bashar al-Assad.
-
Ripoti: Watawala wa kigaidi Syria wanafanya maangamizi ya kizazi katika mji wa Kikristo
Dec 29, 2024 23:43Shirika moja la kutetea haki za binadamu linasema Wakristo wametishwa na kundi la wanamgambo wa Hay'at Tahrir al-Sham (HTS) kuuhama mji wa Maaloula, kusini magharibi mwa Syria, katika kile kinachotajwa kuwa ni kitendo cha maangamizi ya kizazi.
-
Vikosi vya Yemen vyaangusha ndege ya kivita isiyo na rubani ya Marekani MQ-9 Reaper
Dec 29, 2024 23:38Vikosi vya Jeshi la Yemen vimetangaza kuangusha ndege ya kivita isiyo na rubani ya Marekani, aina ya MQ-9 Reaper, katika anga ya mkoa wa Al-Bayda.
-
Mtoto mchanga wa tano afariki dunia Ghaza kutokana na baridi kali na kukosekana kwa vifaa
Dec 29, 2024 09:32Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi wa Kipalestina UNRWA ametoa indhari kuhusu vifo vya watoto Wapalestina vinavyoongezeka kutokana na baridi kali na kukosekana kwa vifaa vya kutosha.
-
Ahadi ya Al-Joulani ya kushirikisha Wasyria wote katika uendeshaji nchi imethibiti kuwa ni uongo
Dec 29, 2024 07:32Kwa kuanza kwa wimbi la timuatimua ya maafisa wa jamii ya Maalawi katika wizara za serikali ya Syria, imethibiti kuwa ahadi alizokuwa ametoa Abu Muhammad Al-Jolani za kutotengwa tabaka lolote la jamii ya Wasyria katika uendeshaji nchi ni za uongo.