-
Kukatwa kikamilifu uhusiano wa Colombia na utawala wa Kizayuni; kuendelea kutengwa Tel Aviv kimataifa
May 02, 2024 23:13Rais Gustavo Petro wa Colombia alisema siku ya Jumatano tarehe Mosi Mei katika hotuba yake kwa mnasaba wa maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani (Mei Mosi) kuwa kuanzia Alhamisi amekata kikamilifu uhusiano wa nchi hiyo na utawala wa Kizayuni kwa sababu ya jinai na mauaji ya kimbari yanayofanywa na utawala huo huko Ukanda wa Gaza.
-
Baada ya uamuzi wa kihistoria wa Colombia; Hamas yataka mataifa yote kuvunja uhusiano na Israel
May 02, 2024 08:16Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS imepongeza na kukaribisha kwa mikono miwili uamuzi wa Colombia wa kuvunja uhusiano wake na utawala haramu wa Israel.
-
Colombia yaamua kuvunja uhusiano na Israel kwa sababu ya mauaji ya kimbari ya Ghaza
May 01, 2024 23:55Colombia imeamua kuvunja uhusiano wake wa kidiplomasia na utawala wa Kizayuni wa Israel kutokana na vita vya kinyama na mauaji ya kimbari yanayoendelea kufanywa na utawala huo haramu dhidi ya Wapalestina wa Ukanda wa Ghaza.
-
Utawala wa Kizayuni umewatia nguvuni mamia ya wafanyakazi wa Kipalestina
May 01, 2024 23:06Vyanzo vya habari vya Palestina vimeripoti kuwa Wazayuni maghasibu wamewatia mbaroni zaidi ya wafanyakazi elfu tano wa Kipalestina katika mwaka huu wa 2024 huku hali za kiafya za raia hao wa Kipalestina zikitajwa kuwa mbaya.
-
Jitihada za China za kuleta maridhiano ya kitaifa Palestina
May 01, 2024 23:05Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China ametangaza kuwa kufuatia mkutano wa wawakilishi wa harakati za Palestina za Hamas na Fat'h mjini Beijing, pande mbili zimefikia makubaliano ya kujadili maridhiano ya kitaifa huko Palestina.
-
Congress ya Marekani inatumika kama ngao ya kumlinda Netanyahu
May 01, 2024 08:10Katika hali ambayo Baraza la Mawaziri la utawala wa Kizayuni lina wasiwasi mkubwa kuhusiana na uwezekano wa kutolewa waranti wa kukamatwa Benjamin Netanyahu Waziri Mkuu na maafisa wengine wa utawala wa Kizayuni, tovuti ya habari ya Axios imeripoti kwamba wajumbe wa Congress wameionya Mahakama ya Kimataifa ya Jinai ICC na kuitaka isitoe vibali vya kutiwa nguvuni maafisa wa utawala wa Israel.
-
Miili 10,000 iliyozikwa chini ya vifusi vya Gaza, inaoza na kueneza magonjwa
May 01, 2024 00:33Shirika la Ulinzi wa kiraia la Gaza limeonya kuhusu maafa ya kiafya yanayokuja katika Ukanda uliozingirwa kutokana na kuoza maiti zilizo chini ya vifusi vya majengo yaliyoharibiwa na mashambulizi ya mabomu ya utawala katili wa Israel.
-
Kukaribia muda wa kutolewa hukumu ya mahakama mbili za kimataifa dhidi ya utawala wa Kizayuni
Apr 30, 2024 22:53Sambamba na kuongezeka uwezekano wa Mahakama ya Kimataifa ya Haki ICJ kutoa hukumu ya kukamatwa maafisa kadhaa wa utawala wa Kizayuni kwa tuhuma za kufanya jinai za kivita huko Gaza, gazeti la Times lilimeandika kuwa, kuna uwezekano pia kwamba Mahakama ya Kimataifa ya Jinai ICC inajiandaa kutoa hati ya kukamatwa Netanyahu na maafisa wengine wa ngazi za juu wa Israel akiwemo Waziri wa Vita, Mkuu wa Majeshi na baadhi ya maafisa wa usalama wa utawala huo kwa kuhusika na vita hivyo.
-
Ujumbe wa Hamas umeondoka Cairo kwa ajili ya mashauriano zaidi
Apr 30, 2024 07:42Ujumbe wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) umeondoka Cairo, mji mkuu wa Misri ili kufanya mashauriano zaidi kuhusu pendekezo jipya lililotolewa kwa ajili ya kubadilishana mateka.
-
Vituo vya utafiti vya Ulaya vyaiunga mkono Palestina na kuiwekea vikwazo Israel
Apr 30, 2024 07:41Vituo vya utafiti barani Ulaya vimeuwekea vikwazo utawala wa Kizayuni na kuunga mkono malengo ya Palestina. Viituo hivyo vya utafiti vya Ulaya pia vimelaani jinai za utawala huo unaotekeleza mauaji ya kimbari dhidi ya watu wa Gaza.