-
Balozi zote za Israel zawekwa kwenye hali ya tahadhari kuhofia waranti wa ICC wa jinai za vita vya Ghaza
Apr 29, 2024 23:17Wizara ya Mambo ya Nje ya utawala wa Kizayuni wa Israel imeziagiza balozi zake duniani kote kuwa tayari kwa madhara yanayoweza kutokea iwapo Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC) itatoa waranti wa kukamatwa maafisa wa utawala huo kwa uhalifu wa kivita na ukiukaji wa haki za binadamu dhidi ya Wapalestina katika Ukanda wa Ghaza.
-
Wapalestina zaidi ya 8,500 wametiwa nguvuni Ukingo wa Magharibi tangu Oktoba 7 hadi sasa
Apr 29, 2024 23:16Jumuiya ya kushughulikia mateka wa Kipalestina imetangaza katika ripoti yake kwamba utawala ghasibu wa Kizayuni wa Israel umewatia nguvuni Wapalestina 8,505 katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan tangu tarehe 7 Oktoba 2023 mara baada ya kutekelezwa operesheni ya Kimbunga cha Al-Aqsa.
-
Kuharibiwa Gaza; Jinai za utawala wa Kizayuni dhidi ya kizazi cha sasa na kijacho
Apr 29, 2024 23:14Mwezi wa saba wa vita unamalizika tangu utawala wa Kizayuni uanzishe vita na mauaji ya kimbari dhidi ya Ukanda wa Gaza, huku mashambulizi ya kila siku ya utawala huo yakisababisha maafa na uharibifu mkubwa wa miundombinu ya mji na afya katika ukanda huo.
-
Wanajeshi 14 wa Israel waangamizwa, wajeruhiwa katika operesheni ya muqawama Gaza
Apr 29, 2024 07:49Takriban wanajeshi watatu wa utawala katili wa Israel wameangamizwa na wengine 11 kujruhiwa vibaya katika eneo la vita kati kati mwa Ukanda wa Gaza, huku vikosi vya muqawama au mapambano ya Kiisalmu Palestina vikiendelea kulisababishia hasara kubwa jeshi katili la utawala huo.
-
UNRWA: Takriban watoto 17,000 wametenganishwa na familia zao Gaza kufuatia vita vya Israeli
Apr 29, 2024 07:33Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi wa Kipalestina (UNRWA) limebainisha wasiwasi wake juu ya hali inayozidi kuzorota ya watoto wa Kipalestina katika Ukanda wa Gaza, huku Israel ikiendeleza vita vyake vya mauaji ya kimbari dhidi ya eneo hilo linalozingirwa.
-
Rais wa Syria: Mshikamano wa nchi za Kiarabu unapelekea kupatikana utulivu katika eneo
Apr 28, 2024 23:36Rais wa Syria amesema kuwa kuwepo mshikamamo baina ya nchi za Kiarabu na kutekeleza hatua za pamoja kutapelekea kupatikana amani na uthabiti katika eneo.
-
Abbas: Utawala wa Kizayuni umeangamiza asilimia 75 ya Ukanda wa Gaza
Apr 28, 2024 23:07Rais wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina amesema kuwa utawala wa Kizayuni wa Israel umeangamiza asilimia 75 ya nyumba, miundombinu ya barabara, vyuo vikuu, misikiti na miundo msingi mingine ya Ukanda wa Gaza.
-
Viongozi wa makundi ya Palestina wakutana Istanbul, Uturuki kujadili yanayojiri Ghaza
Apr 28, 2024 08:23Viongozi wa Harakati za Hamas, Jihadul-Islami na Vuguvugu la Wananchi la Ukombozi wa Palestina wamekutana kujadili yanayojiri kwenye medani za mapambano na za kisiasa za Palestina na vita katika Ukanda wa Ghaza.
-
Uwezekano wa ICC kutoa waranti wa kukamatwa Netanyahu kwa mauaji ya Ghaza umeitia tafrani Israel
Apr 28, 2024 08:15Baraza la mawaziri la utawala haramu wa Kizayuni wa Israel limeingiwa na tafrani na wasi wasi mkubwa juu ya uwezekano wa Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC) kutoa waranti wa kukamatwa waziri mkuu wa utawala huo Benjamin Netanyahu na maafisa wengine waandamizi kwa kuhusika na jinai za vita vya miezi kadhaa vya mauaji ya kimbari dhidi ya Wapalestina wa Ukanda wa Ghaza uliozingirwa.
-
Kushadidi mgogoro wa kisiasa katika baraza la mawaziri la utawala wa Kizayuni
Apr 28, 2024 07:22Kuendelea maandamano ya mitaani huko Palestina inayokaliwa kwa mabavu (Israel), tofauti za kimtazamo kati ya wapinzani na baraza la mawaziri na kuongezeka uwezekano wa Mahakama ya Kimataifa ya Uadilifu kutoa amri ya kumkamata Benjamin Netanyahu kumezidisha mzozo wa kisiasa huko Tel Aviv.