-
Haniyeh awataka Wapalestina kuandamana kwenye Msikiti wa Al-Aqsa siku ya 1 ya Ramadhani
Feb 29, 2024 08:37Mkuu wa Ofisi ya Siasa ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (HAMAS) amewataka Wapalestina katika Ukingo wa Magharibi unaokaliwa kwa mabavu na Israel kuandamana hadi Msikiti wa Al-Aqsa katika siku ya kwanza ya mwezi mtukufu wa Ramadhani.
-
Lolwah Al-Khater: Hatua za utawala wa Kizayuni wa Israel Gazah ni mauaji ya kimbari
Feb 28, 2024 23:32Lolwah Al-Khater, Waziri wa Ushirikiano wa Kimataifa wa Qatar amesema kuwa, jinai za utawala wa Kizayuni wa Israel katika Ukanda wa Gazah ni kielelezo cha wazi cha mauaji ya kimbari.
-
Amir wa Qatar asisitiza ulazima wa kusitishwa jinai za utawala wa Kizayuni Ukanda wa Gaza
Feb 28, 2024 08:20Amir wa Qatar amesisitiza kuwa kuna ulazima wa kusitishwa jinai za utawala wa Kizayuni dhidi ya Ukanda wa Gaza.
-
Hamas: Washington inabeba dhima ya kifo cha mwanajeshi aliyejichoma moto nje ya Ubalozi wa Israel huko Washington + video
Feb 27, 2024 09:13Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina, Hamas, imesema serikali ya Marekani inabeba dhima ya kifo cha mwanajeshi wa nchi hiyo aliyejichoma moto nje ya Ubalozi wa Israel huko Washington akipinga uungaji mkono wa serikali ya Rais Joe Biden kwa mauaji ya kimbari yanayoendelea kufanywa na Israel huko Ukanda wa Gaza.
-
Yemen: Mashambulizi katika Bahari ya Sham yatakoma pale tu Israel itakapositisha vita Gaza
Feb 27, 2024 23:22Msemaji wa Harakati ya Ansarullah inayotawala Yemen amesema mashambulizi ya nchi hiyo ya Kiarabu dhidi ya meli za maadui katika Bahari ya Sham yatakoma tu baada ya utawala wa Israel kuhitimisha vita na mzingiro wake dhidi ya Wapalestina katika Ukanda wa Gaza.
-
OIC yaziomba nchi zote duniani zisiuuzie silaha utawala wa Kizayuni wa Israel
Feb 27, 2024 07:50Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC) amezitaka nchi zote duniani kuacha kutuma silaha na zana za kijeshi kwa utawala unaofanya mauaji ya kimbari wa Israel.
-
HAMAS: Historia katu haitasahau hatua za fedheha za Biden
Feb 27, 2024 03:57Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (HAMAS) amesema historia kamwe haiwezi kufuta hatua ya kufedhehesha ya utawala wa Rais Joe Biden wa Marekani ya kushirikiana na utawala wa Kizayuni wa Israel katika mauaji yake ya kimbari dhidi ya Wapalestina wa Ukanda wa Gaza.
-
Kauli moja ya mirengo ya kisiasa ya Iraq kuhusu wajibu wa kuondoka wanajeshi wa kigeni nchini mwao
Feb 26, 2024 23:01Qasim al-Araji, Mshauri wa Usalama wa Taifa wa Iraq amesisitiza kuwa mirengo yote ya kisiasa ya nchi hiyo yanakubaliana kwa kauli moja kuhusu wajibu wa kuondoka wanajeshi wa kigeni nchini humo.
-
Mkuu wa UNRWA: Janga la njaa la 'kutengezwa na watu' Ghazza linaepukika kwa kuruhusu kuingizwa misaada
Feb 26, 2024 08:17Kamishna Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi wa Kipalestina (UNRWA) amesema baa la njaa kali lililozagaa katika Ukanda wa Gaza linaweza kuepukwa ikiwa misaada itaruhusiwa kuingizwa katika eneo hilo.
-
Waziri wa Ulinzi wa Yemen: Zama za Marekani na waitifaki wake 'kuhodhi' maji ya kimataifa zimekwisha
Feb 26, 2024 07:58Waziri wa Ulinzi wa Yemen amepongeza operesheni za majini zinazoendelea kufanywa na jeshi la nchi hiyo dhidi ya meli zenye uhusiano na utawala wa Kizayuni wa Israel katika Bahari Nyekundu kwa lengo la kupinga vita dhidi ya Ghazza, na kusisitiza kwamba zama za "satua ya kuhodhi" Marekani na washirika wake maji ya kimataifa zimekwisha.