-
Waziri Mkuu wa Pakistan: Uvamizi dhidi ya Iran ndio sababu kuu ya mgogoro wa kikanda
Sep 01, 2026 14:17Waziri Mkuu wa Pakistan, Shehbaz Sharif, amesema kuwa ukiukaji wa mamlaka ya kujitawala na ardhi ya Iran mapema mwaka huu umesababisha mgogoro mkubwa wa kikanda, na kusisitiza kuwa diplomasia ndiyo njia pekee endelevu ya kutatua mgogoro huo.
-
Ripoti za UN: Mashambulizi ya walowezi huko Palestina yanaongezeka, na takwimu zinamkadhibisha Netanyahu
Sep 01, 2026 03:11Kwa wiki ya nne mfululizo, walowezi wa kuzayuni wa Israel wanaendelea kuzingira familia tatu za Wapalestina katika eneo la Ras al-Ain la mji wa Qusra, kusini mwa Nablus, huku mashambulizi yakiendelea dhidi ya nyumba na ardhi za kandokando ya mji huo.
-
Maulama wa Pakistan: Umoja wa Waislamu mkabala wa mashambulizi ya Marekani na Israel si jambo la kupuuzwa
Aug 31, 2026 11:13Kongamano la kila mwaka lenye kaulimbiu ya “Kumpenda Mtume Mtukufu; Kitovu cha Umoja wa Waislamu” limefanyika mjini Islamabad Pakistan sambamba na maadhimisho ya kumbukumbu ya kuzaliwa Mtume Mtukufu wa Uislamu, Muhammad al-Mustafa (SAW), na Wiki ya Umoja.
-
Hizbullah: Marekani na Israel zimeshindwa katika vita vitatu vya uchokozi dhidi ya Iran kutokana na umoja na ustahimilivu wa wananchi
Aug 31, 2026 04:39Katibu Mkuu wa Harakati ya Muqawama ya Lebanon Hizbullah amesifu na kupongeza ustahimilivu na istiqama ya matabaka mbalimbali ya wananchi wa Iran wakati wa vita vya hivi karibuni vya uchokozi vilivyoanzishwa na Marekani na Israel dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu, na kusisitiza kuwa istiqama ya wananchi itawarudisha nyuma maadui na kufelisha njama zao.
-
Waziri wa kizayuni aeleza 'anavyofurahishwa' na mateso wanayopata wafungwa Wapalestina
Aug 30, 2026 13:28Waziri wa usalama wa ndani wa utawala wa kizayuni wa Israel, Itamar Ben-Gvir, amesema "anafurahishwa" na unyanyasaji wa wafungwa Wapalestina walioko kwenye jela za utawala huo na kuongeza kwamba yeye anahusika moja kwa moja na hali zinazoshuhudiwa katika jela hizo.
-
Afrika Kusini yawasilisha kesi ICJ dhidi ya Israel kwa kukataa kutekeleza maamuzi yake kuhusu Gaza
Aug 30, 2026 03:42Afrika Kusini imewasilisha hati mpya ya ushahidi kwa Mahakama ya Kimataifa ya Haki (ICJ), ikiishutumu Israel kwa kukataa kufuata maagizo matatu ya kisheria kuhusu Ukanda wa Gaza, na kuonya kwamba kuendelea ukiukwaji wa sheria za kimataifa kunaweza kudhoofisha himaya inayotolewa na mahakama hiyo na uhalali wake.
-
Sheikh Naim Qassim: Hizbullah imefelisha mpango wa ‘Israel Kubwa’ na kuzuia upanuzi wake ndani ya Lebanon
Aug 29, 2026 10:43Wanamapambano wa harakati ya Hizbullah ya Lebanon wamefanikiwa kuzima njama iliyopewa jina la "Israel Kubwa" na kuzuia upanuzi wa Israel hadi Lebanon. Haya yamesemwa na Katibu Mkuu wa harakati hiyo ya Lebanon.
-
Saudia yashikilia msimamo wake: Hatutoanzisha uhusiano na Israel kabla ya kuasisiwa kwanza nchi huru ya Palestina
Aug 28, 2026 03:24Saudi Arabia imesisitiza kwamba haitaanzisha uhusiano wa kidiplomasia na utawala wa kizayuni wa Israel bila ya kuasisiwa kwanza nchi huru ya Palestina katika eneo la mipaka ya mwaka 1967, na Baitul Muqaddas Mashariki ukiwa ndio mji mkuu wake.
-
Israel inanyakua maelfu ya ekari za ardhi ya Wapalestina katika Ukingo wa Magharibi
Aug 27, 2026 11:52Mamlaka za utawala wa Kizayuni wa Israel zimetwaa maelfu ya ekari za ardhi ya Wapalestina katikati mwa Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan unaokaliwa kwa mabavu ili kujenga kile kinachoitwa "njia ya usalama" kuzunguka vitongoji haramu vya Wazayuni kinyume cha sheria za kimataifa na maazimio ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.
-
Amani ya Kudumu Katika Eneo Itapatikana tu Pale Utawala wa Kizayuni Utakapopokonywa Silaha za Nyuklia
Aug 27, 2026 06:12Madamu silaha za nyuklia za utawala wa Kizayuni wa Israel, ambao ndio utawala pekee unaomiliki silaha za nyuklia katika Asia Magharibi, zitaendelea kufunikwa na utata wa makusudi wa utawala huo pamoja na kimya cha kimataifa, mjadala wowote kuhusu upokonyaji silaha katika eneo hautakuwa na maana na utaendelea kuwa ni unafiki mtupu.