-
Watoto wachanga 14 wafariki katika ajali ya moto iliyotokea hospitalini Pakistan
Aug 26, 2026 11:15Watoto wachanga wasiopungua14 wamefariki dunia katika moto uliozuka kwenye chumba cha watoto cha hospitali ya serikali katika mji mkuu wa Pakistan, Islamabad, huku Waziri Mkuu Shehbaz Sharif akitangaza kuwa ameshaamuru uchunguzi ufanyike kuhusu ajali hiyo.
-
Baada ya miaka 25, Misri yamtambulisha tena mtoto Muhammad al-Durra kwenye mtaala wa somo la historia
Aug 26, 2026 11:13Miaka 25 baada ya tukio lililoishtua na kuitikisa dunia, picha ya mtoto wa miaka 12 wa Kipalestina Muhammad al-Durra aliyeuliwa kinyama na hadharani na jeshi la utawala wa kizayuni wa Israel imehama kutoka kwenye skrini za televisheni hadi kwenye kurasa za kitabu cha kiada cha Misri, katika somo linaloangazia Intifadha ya Pili ya Wapalestina ya mwaka 2000.
-
Je, Vita vya Marekani Dhidi ya Iran Vimesababisha Vipi Nakisi ya Bajeti katika Uchumi wa Qatar?
Aug 26, 2026 06:52Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) limeripoti kupungua kwa takriban asilimia 9 ya uchumi wa Qatar, ambapo baadhi ya wachambuzi wanakadiria kuwa uchumi wa nchi hiyo utapungua kwa asilimia 13 hadi 14 kufikia mwishoni mwa mwaka huu.
-
Pakistan yaripoti 'maendeleo makubwa' katika mazungumzo ya Tehran ili kupunguza mvutano kati ya Marekani na Iran
Aug 25, 2026 10:18Pakistan imeripoti "maendeleo makubwa" katika mazungumzo ya kidiplomasia ya ngazi ya juu yaliyofanyika Tehran, yenye lengo la kupunguza kasi ya vita vinavyoendelea kati ya Marekani na Iran na kuokoa Mkataba wa Maelewano wa Islamabad (MoU), unaosimamiwa na Pakistan.
-
Ripota Maalumu wa UN atoa wito wa kupelekwa haraka kikosi cha kimataifa cha kulinda Wapalestina Ukingo wa Magharibi na Gaza
Aug 24, 2026 13:34Ripota Maalumu wa Umoja wa Mataifa kuhusu Haki za Binadamu katika Maeneo Yanayokaliwa kwa ya Palestina, Francesca Albanese, ametoa wito wa kupelekwa haraka kikosi cha kimataifa cha kuwalinda Wapalestina katika Ukingo wa Magharibi unaokaliwa kwa mabavu na Ukanda wa Gaza.
-
Kamanda Qaani: Palestina ni fikra iliyo hai na isiyobadilika
Aug 24, 2026 06:08Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu nchini Iran amesema: "Suala la kukomboa Palestina, kuanzia baharini hadi mtoni, (ardhi ya Palestina kuanzia Bahari ya Mediterania hadi Mto Jordan) liko hai zaidi na linawezekana kutimizwa sasa kuliko hapo awali."
-
Hamas yawapongeza mabalozi wa zamani wa Ufaransa na Uingereza wanaotaka Israel iwekewe vikwazo
Aug 23, 2026 13:57Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (HAMAS) imepongeza muungano wa wanadiplomasia zaidi ya 100 wa zamani wa Ufaransa na Uingereza wanaozitaka serikali za nchi zao kushirikiana kulinda sheria za kimataifa katika maeneo yanayokaliwa kwa mabavu ya Palestina. Mabalozi hao pia wametaka Israel iwekewe vikwazo.
-
Mwisho wa satwa ya Marekani: Asia Magharibi Katika Ukingo wa Mfumo Mpya
Aug 23, 2026 06:27Katika uchambuzi wake wa hivi karibuni, jarida la Foreign Affairs linataja vita dhidi ya Iran kama hatua muhimu inayoharakisha kuporomoka kwa mfumo wa kikanda unaoongozwa na Marekani na kudhihiri taratibu mabadiliko yanayoweza kubadili mitazamo na mikakati ya kiusalama ya mataifa ya Asia Magharibi katika miaka ijayo.
-
Vitisho Visivyo na Uzito vya Trump na Kudhoofika kwa Nguvu ya Marekani
Aug 23, 2026 04:57Rais Donald Trump wa Marekani kwa mara nyingine tena ametishia kuishambulia Oman kwa mabomu, nchi iliyo na nafasi muhimu katika mazungumzo yanayohusu Iran pamoja na masuala yanayohusiana na usafiri wa baharini katika Lango Bahari la Hormuz.
-
Maafisa wa jeshi la Israel: Netanyahu anataka kushadidisha vita ili uchaguzi usifanyike
Aug 23, 2026 03:12Maafisa waandamizi wa jeshi la utawala wa kizayuni wa Israel wanamshuku waziri mkuu Benjamin Netanyahu kwamba anaweza akataka kushadidisha vita katika Ukanda wa Ghaza ili kujaribu kuvuruga au kuahirisha uchaguzi ujao wa bunge wa utawala huo ghasibu.