Mkutano wa kilele wa BRICS nchini Afrika Kusini
Mkutano wa siku tatu wa wakuu wa nchi tano za BRICS na uwepo wa makumi ya wakuu wengine wa nchi ulianza huko Johannesburg, Afrika Kusini mnamo Jumanne, Agosti 22, 2023.
Huu ni mkutano wa 15 wa viongozi wa BRICS ambao uahudhuriwa na Rais Luiz Inacio Lula da Silva wa Brazil, Rais Xi Jinping wa China na Waziri Mkuu wa India Narendra Modi. Rais Vladimir Putin wa Russia atawakilishwa na Waziri wa Mambo ya Nje, Sergey Lavrov. Mwezi Machi, Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) ilitoa hati ya kukamatwa Putin, ambayo ilimzuia kusafiri kuhudhuria mkutano huo, ambao umepangwa kufanyika kuanzia
Mada kuu katika mkutano huu ni kujiunga wanachama wapya pamoja na njia za kupanua ushawishi wa kisiasa na kiuchumi wa kimataifa wa BRICS. Nchi 23 zimewasilisha rasmi maombi ya kujiunga na BRICS. Orodha hiyo inaonyesha wapi BRICS inaelekea kwa kuwakubali, kwani nchi zilizowasilisha maombi ni pamoja na Saudi Arabia na Umoja Falme za Kiarabu hadi Argentina na Iran, Cuba, Belarus na Venezuela.
Mahitaji ya pamoja ya wanachama wa BRICS, ambao huzalisha robo ya utajiri wa dunia na kujumuisha asilimia 42 ya watu wote duniani, "ni kuletauwiano unaojumuisha zaidi masuala ya kisiasa na kiuchumi duniani, hasa dhidi ya Marekani na Umoja wa Ulaya."
Wakati China, Russia, India, Brazil na Afrika Kusini, zikiwa nchi zinazoinukia kiuchumi, ni wanachama wa BRICS, kundi hili linajaribu kuongeza nchi wanachama na kupanua ushawishi wake duniani." Rais wa China Xi Jinping katika makala iliyochapishwa Jumatatu katika vyombo vya habari vya Afrika Kusini vilisema: "Viongozi wa nchi za BRICS katika mkutano huu wa kilele wanataka jumuiya ya kimataifa "kuzingatia jukumu kubwa la utaratibu wa ushirikiano wa BRICS katika utawala wa kimataifa."
Wataalamu wa nchi za Magharibi wanajaribu kuibua suala la kuandikisha wanachama wapya kwa BRICS kama chanzo cha mifarakano katika kundi hili. Wanadai kuwa suala la upanuzi wa BRICS linabishaniwa haswa kati ya India na Uchina, nchi mbili zenye nguvu kiuchumi za kundi hili. Waziri wa Mambo ya Nje wa Afrika Kusini alisema Jumapili kwamba nchi hiyo inafanyia kazi orodha ya "miongozo" kwa wanachama wapya kuingia mwaka huu.
Mnamo mwaka wa 2009, madola yanayoibukia na uchumi wa dunia yalijaribu kuanzisha umoja wa kisiasa na kiuchumi kwa ushirikiano bila ya uwepo wa nguvu za Magharibi na hapo ndipo BRICS ilipozaliwa. China na Russia zikiwa nchi zenye ushawishi mkubwa katika BRICS zinataka kukomesha satwa na nguvu za kiuchumi za nchi za Magharibi katika uhusiano wa kibiashara. Wanachama wa BRICS pia wameelezea mara kwa mara hamu yao ya kutaka uwakilishi ufaao zaidi wa nchi zinazostawi katika taasisi za kimataifa kama vile Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, Shirika la Fedha la Kimataifa au Shirika la Biashara Duniani. Kundi la BRICS ni kielelezo cha nia ya nchi tano wanachama wake, nne kati yao ni China, India, Brazil na Afrika Kusini, ambazo ni nchi zinazoinukia kiuchumi, kushiriki katika usimamizi wa uchumi wa dunia na kushindana dhidi ya Kundi la G7 la nchi zilizostawi kiviwanda.
Ushawishi wa BRICS umekuwa mkubwa kiasi kwamba mara nyingi hulinganishwa na G7. Ingawa, baadhi ya vigezo vya ulinganisho vinaweza kuwa sahihi, makundi haya mawili kimsingi yanatofautiana katika suala la madhumuni, muundo na mageuzi. Kikundi cha G7 kinafanana kisiasa, kiuchumi na kiitikadi, wakati BRICS ni tofauti katika mambo yote. Jukumu la Kundi la G7 ni kudumisha utaratibu wa zamani ambapo nchi za Magharibi zilitawala wakati BRICS kwa kukubali wanachama wapya inataka kuunda utaratibu mpya wa dunia.
Wakati huo huo, BRICS inataka kubadili mfumo wa dunia hasa uchumi wa dunia.Urusi inataka wanachama wa BRICS kuchukua hatua madhubuti katika kurekebisha mfumo wa fedha na uchumi wa dunia, ili masharti ya maendeleo na ukuaji wa uchumi wa nchi zinazoendelea uwe mazingira ya usawa.
Rais wa Russia Vladimir Putin amependekeza kuwa wanachama wa kundi la BRICS wachukue hatua kikamilifu kurekebisha mfumo wa fedha na uchumi wa dunia ili kuandaa mazingira ya usawa katika maendeleo na ukuaji wa uchumi wa nchi zinazoendelea.
BRICS ilianza shughuli zake miaka 14 iliyopita kwa lengo la kuimarisha mahusiano ya kibiashara na kiuchumi ya nchi zinazoendelea na pia kuunda taasisi mpya za kimataifa kama vile benki za maendeleo na mfumo mpya wa biashara. BRICS ina uwezo muhimu sana wa maendeleo kuongeza kasi ya kiuchumi na kuwa nguzo yenye ushawishi na maamuzi katika uchumi wa kimataifa.