Aug 27, 2023 13:12 UTC
  • Rais wa Brazil atoa mwito tena wa kufanyiwa mageuzi Baraza la Usalama la UN

Rais Luis Inacio Lula da Silva wa Brazil amerudia tena wito wake wa kufanyiwa mageuzi Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.

Lula da Silva ametoa wito huo katika mkutano na waandishi wa habari huko Luanda, mji mkuu wa Angola, ambapo mbali na kutaka yafanyike mageuzi katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa amebainisha kwamba badala ya kuwa mdhamini wa usalama, amani na utulivu, Baraza la Usalama linaeneza vita duniani.
 
Rais wa Brazil amesema, Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lazima liendane na hali halisi ya hivi sasa duniani na kubainisha kuwa taasisi hiyo ya kimataifa imedhoofika; na muundo wa sasa wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa haukidhi tena malengo liliyoundiwa.
Baraza la Usalama la UN

Kwa mujibu wa Lula da Silva katika mwaka 2023 Umoja wa Mataifa umejiweka mbali sana na itibari uliyokuwa nayo mwaka 1945.

 
Rais wa Brazil jana alikamilisha safari yake ya siku mbili nchini Angola kisha leo Jumapili ameendelea na ziara yake barani Afrika kwa kuitembelea nchi ya Sao Tome and Principe ambako atahudhuria pia mkutano wa 14 wa viongozi wa jumuiya ya nchi zinazozungumza Kireno.../

Tags